Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy
Mwalimu (katikati) akiwa katika ziara
kukagua soko la Temeke la Stereo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya
Temeke Protidas Kagimbo.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy
Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni Injinia Mussa Natty.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy
Mwalimu akipata maelezo juu ya usafi wa mazingira eneo la soko unavyofanyika.
Anayetoa maelezo ni Mwenyekiti wa Soko la Tandale Sultan Ally Kinombo.
*******
Halmashauri zote Nchini zimetakiwa kuendelea kuhamasisha na
kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya utunzaji
wa mazingira na pia kuimarisha
miundombinu ya masoko ambayo ni mibovu na ya kizamani. Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati
alipofanya ziara ya kutembelea masoko ya manispaa za Temeke na Ilala za jijini
Dar es Salaam.
Amekumbushia pia kila Manispaa kuzingatia agizo la Makamu wa
Rais la kufanya usafi kila jumamosi ya mwanzo wa mwezi pia ametoa wito watu
kutooneana aibu katika kutupa taka hovyo. Kila mtu awe mlinzi wa mwenzie
kuhakikisha anatunza mazingira ianavyotakiwa na pia hatupi taka hovyo, alisema
Mheshimiwa Ummy.
Katika ziara hiyo aliongea na wafanyabiashara katika masoko
hayo na walimwambia changamoto wanazokutana nazo katika swala zima la
kudumisha usafi katika sehemu zao za
biashara ni uhaba wa maji na vifaa vya kufanyia usafi.
Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za mbalimbali za Viongozi
wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira unafanikiwa
kwa kiasi kikubwa katika jiji la Dar es Salaam na Nchi ya Tanzania kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment