Nafasi Ya Matangazo

October 06, 2014

SAM_0064
Mhifadhi wa Utalii wa
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Eva Mallya akizungumza
 katika ziara ya waandishi wa habari kutoka Arusha walikwenda kutembelea
hifadhi hiyo na kujionea shughuli  mbalimbali za utalii ikiwemo
kivutio cha kupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima pekee mrefu na kilele chake kina
Barafu Barani Afrika.
SAM_0010
Baadhi ya sehemu ya waandishi wa habari
SAM_0058
 SAM_0066Muonekano ndani ya ukumbi wa mkutano katika makao makuu ya KINAPA
SAM_0074Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima Grace Macha akifanya mahojiano na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65)ambaye  ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro
SAM_0054Mmiliki wa mtandao wa jamiiblog Pamela Molle wakiwa anasalimiana na mwandishi mwandamizi wa gazeti la The citizen  Patty Magubira
SAM_0076Mwandishi wa habari Leo Veronicah Mheta akipozi katika picha na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ambaye ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro
SAM_0078
Mwandishi wa Uhuru Lilian Joel akiwaanafanya mahojiano na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro
SAM_0086 

RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ambaye ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa anaonyesha cheti chake mara baada ya kukabidhiwa pembeni ni muongoza watalii KOMBE la Dunia linachangia baadhi ya watalii kushindwa kufika Nchini Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro kutokana na watu mbalimbali kuwa makini na mpira kuliko suala la utalii.

Hayo yalisemwa jana Mkoani Kilimanjaro na  Mhifadhi wa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Eva Mallya wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo kujionea shughuli za  mbalimbali za utalii ikiwemo kivutio cha kupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima pekee wenye Barafu Barani Afrika.

Alisema mashindano ya kombe la Dunia yanapofanyika baada ya miaka mine kupita idadi ya watalii wanaotaka kutembelea vivutio vya utalii inapungua kutokana na watalii hao kupenda kuangalia mpira zaidi.

Alisema ingawa mashindano hayo yanapofanyika yanaleta manufaa kwa kila nchi lakini nchi nyingine zenye kutangaza masuala ya utalii idadi ya wageni inashuka kutokana na wageni wengi kupendelea mpira zaidi.

Alisema hifadhi hiyo inawatalii wa mataifa mbalimbali wanaitembelea kutokana na vivutio vilivyopo vya wanyama, mazingira pamoja na upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambao ni wa kipekee na wenye barafu.

Alisema mwaka  fedha 2011/12 idadi ya wageni kutoka nchi mbalimbali iliongezeka na kufikia 57,456 ambayo ni kubwa zaidi lakini mwaka 2012/13 wageni walikuwa 55,553 huku mwaka 2013/14 walipungua na kufikia  51,286.

Alisema sababu za kupungua kwa watalii wanaofika Kinapa mojawapo ni mashindao ya kombe la Dunia, mtikisiko wa uchumi pamoja na ukosefu wa ajira.

“Kombe la Dunia linachangia wageni kutofika kutembela vivutio vya utalii ndio yanapofanyika mashindano yanafaida zake lakini pia kunasababu mbalimbali ila kwakuwa Mlima Kilimanjaro unajiuza tunapata wageni wa mataifa mbalimbali na pia nawaomba watalii wa ndani na wanachi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) watembelee hifadhi hii ya Kinapa”. (Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Posted by MROKI On Monday, October 06, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo