Rama Salim (kushoto) akiwania mpira na Emmanuel Okwi wa Simba.
Na Fadher Kidevu Blog
KIUNGO wa Coastal Union Mkenya Rama Salim amesema yeye ni zaidi ya
Haruna Niyonzima na Pierre Kwizera wanaochezea klabu kongwe za Simba na Yanga
Rama Salim amesema licha ya
nyota hao kutoka nchi za Burundi na Rwanda kuwa na majina makubwa lakini
wanamchango mdogo kwa timu hizo tofauti na uwezo wao wanapokuwa uwanjani
“Pengine majina yao yanatokana
na ukubwa wa timu wanazochezea lakini uwanjani hawana tofauti nanigumu
kushindana na mimi kwa sababu nimewaacha mbali na kazi yangu inaonekana ndani
ya timu.
Rama Salim amejiunga na
Coastal msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya na tayari ameifungia timu hiyo
bao moja katika mechi dhidi ya Simba ambapo tiu hizo zilitoka sare ya 2-2
kwenye mechi ya ufunguzi ya msimu huu uwanja wa taifa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment