Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2014

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari pamoja na jopo la wanasheria kutoka Marekani (hawapo pichani kuhusu jambo hilo Dar es Salaam leo. 
 Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu jambo hilo. Kulia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Joe Mgaya na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira.
 Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Joe Mgaya. 
 Mwanasheria Respicius Didace akizungumza katika mkutano huo.
 Dk. Isaya Tosiri, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa Fedha na Ugavi, Terevael Masawe akizungumza katika mkutano huo.
 Mwandisi Mwandamizi wa Gazeti la Serikali Daily News, Faustine Kapama akiuliza swali kwa jopo hilo la wanasheria.   
 Justus Selestine kutoa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), akizungumza katika mkutano huo.
 Mwanahabri akichangia hoja.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mgeni mualikwa Lise Heide kulia akifurahia jambo Evelyn Rugemalira katika mkutano huo.
  Mwanasheria maarufu kutoka Amsterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kulia), akiteta jambo na Wakili Okare Joshua (kushoto) na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Benedicta Rugemalira (wa pili kushoto), akiteta jambo na wageni waalikwa.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Benedicta Rugemalira (wa pili kushoto), akiteta jambo na Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitemea, James Rugemalira (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.
 Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wageni kutoka Marekani wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte akizungumza katika mkutano huo.
  Mwanasheria Respicius Didace akiwa amepozi na mke wangu katika mkutano huo.
 Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya VIP Engineering and Marketing Limited imetoa wito kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikari (CAG) na taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) kutoa mapema taarifa ya uchunguzi inayohusiana na uchotwaji wa fedha katika akaunti maalumu ya Escrow Benki Kuu ya Tanzania.

Mwito huo umetolewa na Mshauri ya Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira wakati akiongea na waandishi wa habari pamoja na jopo la wanasheria wa kimataifa kutoka Marekani  waliopo nchini Dar es Salaam jana kwa ziara maalumu.

“Mimi nashangaa kwa nini taarifa hizi hazitoki. Nilitegemea zitoke hata jana. Mimi nimeshatoa maelezo yangu na niko muwazi kwa jambo hili. Nilitegemea taarifa hizi ziwe zimeshatolewa ili wananchi wajue ukweli wa swala hili,” alisema  Rugemalira.

Rugemalira alisisitiza kuwa fedha zote zilizowekwa kwenye akaunti hiyo si mali ya serikali na kwamba kampuni yake iliuza kihalali hisa zake kwa kampuni ya Pan African Power Solutions ambayo inawajibika kwa mujibu wa amri ya Mahakama Kuu kulipa wadai wote wa kampuni ya IPTL.
Akizungumza na waandishi wa habari, wakiri maarufu kutoka Uhi, Dk Camilo Schutte, aliishauri serikali ya Tanzania kuwaeleza ukweli wahisani na wafadhili hapa nchini kuwa fedha zinazobishaniwa si mali ya umma bali ni fedha zinazohusu makampuni binafsi.

Wakili huyo alisikitishwa na kitendo cha wafadhili hao kusitisha ufadhili wa kuunga mkono bajeti ya serikali ya Tanzania kwa kusikiliza maneno ya pembeni kuwa fedha zinazobishaniwa ni mali nya umma. “Seriklali iwaambie watanzanmia ukweli. 

Hizi sio fedha za umma . Ni mali inayohusu makampuni binafsi,” alisisitiza.

Posted by MROKI On Monday, October 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo