LEO watoto
wetu wapatao 808,111 wanamaliza elimu yao ya msngi ya Darasa la Saba nchini
kote.
Hii ni
idadi tu ya wale ambao wamejisajili kufanya mitihani hiyo kwa mawa huu na
Baraza la Mitihani kuwatambua katika takwimu zao hapa nchini kwa mwaka huu wa
2014 lakini huenda vijana waliostahili kumaliza elimu hiyo ingekuwa kubwa zaidi
ukilinganisha na wale waliojindikisha darasa la kwanza 2007.
Nimesema
watoto wetu wanamaliza kwaklua tu na mimi katika hao 808,111 bimnti yangu ni
mmoja wapo wa wanaomaliza leo na kwa enzi zetu sisi wazazazi wao tungejitapa
kuwa ni LY ambayo kimsingi kipindi ile tupo ambao tulikua hatuji maana yake
bali ni kufuata mkumbo tu kutokana na viingereza vyetu vya Ugoko kutoka Shule
ya Msingi Chini ya Mti.
Hahahaaaa!
Mimi nilikuwa nafahamu maana yake ni Last Year! Na hii ni kwasababu tu kaka
zangu walikuwa wananifundisha watokapo likizo.
Hoja yangu
hapa ni juu ya vijana wetu hawa zaidi ya laki nane ambao kesho wanaingia mtaani
na kuazia septemba 12 ni raia na wanarudi mtaani.
Sawa tunaamini
kuwa wengi wao baadae watafaulu na kujiunga tena na elimu ya sekondari kupitia
shule zetu ambazo tumezijenga kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na hata Taifa
kama zipo wataenda. Pia wapo watakao pelekwa na wazazi wao shule za St. Kidevu,
St. Kazamoyo na St Kenya na Uganda kwa elimu zaidi.
Hivi
katika kipindi hiki kifupi cha kusubiri matokeo tunawasaidiaje watoto hawa
kuwajengea misingi bora ya kuishi? Ama tunawatupa tena katika vituo vya masomo
ya ziada (Tution) am,bazo zimezagaa kila kona ilimradi tu wazazi tusikae na
watoto wetu majumbani.
Ndio wapo
wazazi ambao wanasema, Ah! Huyu mtoto asinisumbue akisubiri matokea aende
Pre-form One na akae huko huko shule. Tena mzazi huyu ndo yule ambaye mtoto
wake alikaa shule ya msingi ya bweni kwa miaka 7.
Naimani hiki ndo kipindi cha kukaa na watoto wetu majumbani na kujua tabia zao vyema ambazo wamejifunza huko mashuleni na ikibidi kuzipiga msasa na kuwaweka sawa.
Wale
wenzangu na mimi kutoka shule ya Msingi Kinyenze au Kipera wao ni tofauti maana
huko hakuna cha kupelekwa masomo ya
ziada au nini ni safari ya kwa bibi au kwa babu ama kwenda mijini hasa Dar es
Salaam kwa kaka, mjomba au ndugu wa karibu kuvuta subira ya kusubiri matokeo na
kama hana matumaini ya ufaulu na kuchaguliwa hutafutiwa kazi za ndani au
vibarua vya kuuza maji na pipi mtaani.
Lakini
leo mimi nakumbuka yaliyokuwa yakifanywa miaka yetu na serikali na hili
lilikuwa amri ambayo sijui imeishia wapi yarababi. Hivi nyie mlio hitimu miaka
ya 1980’s huko hadi 90 nadhani mnakumbuka jinsi ambavyo ukimaliza elimu ya
msingi ulikuwa ukifanyiwa.
Ilikuwa
ni jambo la lazima kila mhitimu kuwa na shamba japo la nusu ekari ambalo
umepanda pamba na shamba lingine la ukumbwa huo um,epanda mazao ya chakula.
Hili
najua kwa mijini ilikuwa haliwezekani lakini vijijini kwetu ilikuwa inawezekana
sana na ilikuwa inaleta tija katika jamii maana inawafanya vijana hawa
wasizurule hovyo na kujiingia katika makundi yasiyo faa.
Hii
leo wahitimu wa elimu ya msingi ni watoto sana. Huenda mwenye umri mkubwa kwa
sasa ana miaka 13, bado wadogo sana nadhani sisi kama wazazi ipo njia stahiki
ya kuwasaidia watoto wetu hawa katika kipindi hiki kigumu.
Tulio
mijini na sisi tusiwaite wadogo zetu na ndugu zetu kutoka kijijini kuja mijini
kwa lengo la kuwatafutia shughuli za kufanya kwani bado wadogo sana na
nitafurahi sana kama tutafanya hivyo kwa kuwapeleka katika masomo ya ziada
kujiandaa na kuanza kidato cha kwanza.
Wajifunze
vyema lugha ya mawasiliano huko sekondari ambayo ni kiingereza na mambo mengine
muhimu.
Wazazi
waepuka sana watoto wao kuwa wazurulaji mitaani na badala yake watafutiwe
shughuli za kufanya ili kuepuka kuzalisha vijana wapya wa vijiwebni na watoa
lawama kwa kukosa kazi ilahali wao waliamua kukaa kijiweni.
Wahitimu
wito wangu kwenu ni kuwa wavumilivu na wasikivu kwa wazazi au walezi wenu ili
mambo yaende sawa wakati tukijipanga ni wapi tunaenda.
0 comments:
Post a Comment