Na
Fadher Kidevu Blog
KOCHA
mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mart Nooij ameita kikos cha
wachezaji 26 kwa ajili ya mechi ya kirafiki iliyopo kwenye Kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa ya FIFA dhidi ya Benin ambayo itachezwa Oktoba 12 uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Kocha
Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho
la Mpirawa Miguu Afrika (CAF), amesema mchezo huo ni muhimu kwa Tanzania
kushinda ili kurudisha matumaini kwa mashabiki wake ambao wamekata tamaa baada
ya kutolewa katika mshindano mbalimbali ikiwemo yale ya kufuzu fainali za
mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika Morocco mwakani.
“Benin
ni timu nzuri ambayo itatupa mazoezi mazuri lakini kurudisha imani kwa mashabi
wetu ambao wamepoteza matumaini na sisi,”amesmea Nooij.
Kikosi
hicho kinatarajia kuingia kambini Oktoba 6 na wachezaji walioitwa kwenye kambi
hiyo kwa upande wa makipa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula
(Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki
ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam
(Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo
ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba
(Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna
Chanongo (Simba).
Washambuliaji
ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR
Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane
Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
0 comments:
Post a Comment