Na Magreth
Kinabo,Dodoma
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni
mwanasiasa mkongwe nchini , Mzee Kingunge Ngomabale Mwiru amesema Katiba bora ni ile itakayozingatia historia
mafanikio ya miaka 50 iliyopita
na Muungano imara.
Kauli hiyo
imetolewa leo mjini Dodoma na Mzee Kingunge wakati akichangia katika mjadala wa Bunge hilo juu ya uwasilishaji wa taarifa za Kamati Namba Moja hadi Kamati Namba Kumi
na Mbili za Bunge hilo kuhusu uhakiki wa Rasimu
ya Katiba iliyopendekezwa.
Aidha Mzee
Kingunge amesema wameondosha mapendekezo
ambayo yanataka kusambaratisha muungano ili uweze kuwa imara.
Mzee
Kingunge aliyataja mambo matatu ambayo yatazingatia Katiba bora kuwa ni
ni ile itakayoimarisha historia ya mafanikio ya miaka 50 iliyopita,
inayopunguza na kuondoa kero mbalimbali
za msingi.
Aliongeza kuwa tatu ni “Lazima Katiba Mpya iingize mambo ambayo yataimarisha nafasi za wananchi mfano
wakulima , wafugaji, wavuvi, wasanii na wachimbaji wadogo… Tanzania
haitakuwa kama ilivyokuwa huko nyuma baada
ya mkutano huu.
“ Kwa
sababu makundi yote yote yamekutana hapa kuzungumzia maslahi yao na hatma yao,”
alisema Mzee Kingunge.
Mzee
Kingunge alisema mawazo yaliyotolewa na ni ushindi mkubwa, kazi iliyobaki ni
kupitisha.
“Kazi hii si ndogo ni kubwa…kwani kuna
zogo , lakini
tumevulia napenda iandikwe kwa wino wa dhahabu kama ilivyo hapa ndani,”
alisisitiza.
Mwanasiasa
huyo alifafanua kuwa Katiba ni maridhiano, hivyo anajua wakubwa
wataendelea kuzungumza, hivyo katika hilo ni vizuri wakawa waangalifu.
“ Tuifanye
kazi hii kwa unyenyekevu, wananchi
wanangoja Katiba bora,” alisema.
0 comments:
Post a Comment