Meneja Takwimu Mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi akizungumza na
waandishi wa Habari kuhusu zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda limeloanza
rasmi leo wilayani Ludewa kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda
inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.
Meneja Takwimu Mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi akisisitiza jambo
wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika
leo Mkoani Iringa kuhusu zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda limeloanza
rasmi leo wilayani Ludewa kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda
inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014
********
Na Veronica
Kazimoto, Ludewa
Wito
umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda waliopo katika wilaya ya Ludewa Mkoani
Njombe kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi wakaopita
katika viwanda vyao ili kufanya zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda kwa ajili ya
maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mkoani Iringa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Meneja Takwimu mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi
amesema zoezi hilo linaanza rasmi leo tarehe 25 Agosti, 2014 na litamalizika
siku ya Jumapili tarehe 31 Agosti, 2014.
“Zoezi la
Uorodheshaji wa Viwanda wilaya ya Ludewa linaanza rasmi leo na litahusisha
jumla ya kata kumi na sita ambazo ni pamoja na Ludende, Lugarawa, Ruhuhu,
Lupanga, Lwela, Mavanga na Mundindi”, amesema Fundi.
Amezitaja
kata nyingine kuwa ni, Ibumi, Mlangali, Kilondo, Madope, Lupingu, madilu,
Makonde, Mkongobaki na Lifuma.
Fundi
amefafanua kuwa taarifa zinazokusanywa katika zoezi hili kutoka viwandani ni
pamoja na jina la kiwanda, anuani za kiwanda, mahali kiwanda kilipo, aina ya
umiliki na utaifa wa mmiliki.
Taarifa
nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mwaka kiwanda
kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi na gharama
za uzalishaji.
Zoezi hili la
Uorodheshaji wa Viwanda lilianza tarehe 8 Aprili, 2014 kwa Tanzania Bara na
mpaka sasa karibu maeneo yote zoezi hili limekwisha kamilika.
0 comments:
Post a Comment