Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2014

Na Mwandishi Wetu
KAZI IMEANZA! Shindano la Redd’s Miss Kinondoni, linazidi kushika kasi na kazi kubwa ipo leo wakati atakaposakwa mrembo mwenye kipaji kati ya 20 wanaoliwania taji hilo.
 
Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema warembo hao wataanza mchakato wa kumsaka Redd’s Miss Kinondoni Talent, katika shindano kali zaidi kuliko lote litakalofanyika leo kwenye Ukumbi wa Maisha Club Uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.
 
Husna alisema, shindano hilo la vipaji litakuwa la kipekee kutokana na mengine yote yaliyowahi kufanyika na ana uhakika mkubwa watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake.
 
“Kesho (leo) ni vipaji kwa kwa sasa kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya shindano hilo.”
 
Shindano la Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape 1 uliopo Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na Christian Bella.
 
Taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.
 
Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu.
 
Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu, Glitters Salon, EFM,UhuruMarathon na Habari Mseto Blog.
Posted by MROKI On Thursday, August 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo