Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2014

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu-Joseph Simbakalia akipokea maelezo ya shughuli zinazofanywa na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) na Ukumbi mpya wa Mikutano wa kimataifa wa  Julius Nyerere uliopo Dar es Salaam (JNICC) kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko na Utafiti, Linda Nyanda wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya maonesho ya wakulima Ngongo Mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu-Joseph Simbakalia akingalia taarifa mbalimbalibandani humo. Ambapo pia ameelezwa na Afisa Mkuu wa Masoko na Utafiti, Linda Nyanda, kuwa taasisi hiyo ya serikali iliyochini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, inampango wa kuwekeza katika sekta ya kumbi za mikutano na nyumba mikoa ya kusini na utafiti wa awali bado unafanyika kuona kama kuna uwezekano wa kufanya hivyo. Na mkuu huyo wa Mkoa kuwakaribisha.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu-Joseph Simbakalia akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka bandani humo. wanaoshuhudia ni Afisa Mkuu wa Masoko na Utafiti, Linda Nyanda (kulia) na Afisa Uhusiano na Itifaki wa JNICC, Beatha Hyera.
Afisa Mkuu wa Masoko na Utafiti, Linda Nyanda (kulia) na Afisa Uhusiano na Itifaki wa JNICC, Beatha Hyera wakikabidhi zawadi.
Posted by MROKI On Thursday, August 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo