Sheikh Dlulkifilo Omari kulia akiwa na baadhi ya waumini mara baada ya ibada hiyo leo
Mmoja kati ya waumini wa dini ya Kiislam waumini wa
madhehebu ya answaar Sunna iliyofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa akitoka kuswali leo
********
Na Matukiodaima blog
Sheikh wa msikiti wa Hidaya katika manispaa ya Iringa Dhulkifilo Omary wa amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa jitihada zake kubwa za kufanikisha Tanzania kuanza mchakato wa kupata katiba mpya na kuwaonya wajumbe wa bunge la katiba kurejea bungeni kuunda bora badala ya kuendeleza mivutano isiyo na tija.

Akizungumza leo na mtandao huu wa matukiodaimablog mara baada ya swala ya Idd -el Fitr kwa waumini wa madhehebu ya answaar Sunna iliyofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa Sheikh Omary alisema kuwa kazi kubwa na nzuri imefanywa na Rais Kikwete katika kuanzisha mchakato wa katiba ikiwa ni pamoja na kuunda tume ya katiba na hadi kufanikisha rasmu hiyo ya katiba .
Hivyo alisema kuwa wajibu wa wajumbe wa bunge la katiba na kushiriki kuandaa katiba ambayo italetwa kwa wananchi kwa lengo la kuipigia kura na si wakati wa wajumbe hao kuanza mivutano isiyo kuwa na tija .
" Mimi kwa mawazo yangu mimi kama sheikh Omary hawa wajumbe wa bunge la katiba walipaswa kuketi pamoja bunge na kutuletea katiba nzuri na sio kutuletea vurugu na malumbano yasiyo kwisha katika bunge hilo"
Alisema kuwa vurugu zinazoendelea juu ya katiba hiyo kwa wajumbe kuwa katika makundi makundi ni wazi kuwa hakutakuwa na katiba mpya kwa sana iwapo makundi hayo yataendelea
0 comments:
Post a Comment