Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha(CCM) Namelok Sokoine akimkabidhi
mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Irkisongo wilayani Monduli Happiness
Nyange msaada wake wa shilingi millioni moja kufuatia kuungua kwa
mabweni ya shule hiyo jana.
Mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya Monduli, Paulina Ngoyai(mama
Kalaine) akikabidhi msaada wake wa mifuko mitano ya sementi kwa shule
hiyo.
Mwakilishi wa kiwanda chaTanfoam cha jijini Arusha Sajid
Ibrahim(kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro 100 yenye
thamani ya shilingi millioni 3 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya
Irkisongo Wilayani Monduli Happness Nyange(kushoto), kufuatia mabweni
ya shule hiyo kuteketea kwa moto hapo jana.Msaada huo unatokana na
harambee ya papo kwa papo aliyoifanya mbunge wa Monduli Mh Edward
Lowassa akitumia simu yake ya kiganjani. Wadau kadhaa wa elimu
wamejitokeza kusaidia ambapo mbunge wa Arusha Viti maalum Namelok
Sokoine amechangia shilingi millioni moja.
Mapacha wanaoishi Wakaazi wa New York Marekani Joy na Jane wakimkabidhi
mkuu wa shule hiyo mama Nyange sehemu ya msaada wao wa kilo zaidi ya
kumi za misumar
Mbunge wa Viti maalum(CCM) mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiangalia
bweni la shule hiyo ya Irkisongo wilayani Monduli lililoteketezwa na
moto jana
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Irkisongo wakibeba magodoro hayo
0 comments:
Post a Comment