Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2014

Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Lucy Simbila akizungumza kabla hajamkaribisha Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga afungue Kambi ya Upimaji Afya.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dk. Charles Rweikiza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Wilaya ya Kahama. Kushoto ni Dk.Mzige, wa tatu kutoka kushoto ni  Kaimu Meneja wa NSSF Kahama , Salum Salahange, Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk.Lucy Simbila na Ofisa Uhusiano NSSF, Jumanne Mbepo. 
Dk.Mzige Akitoa Ushauri kwa mmoja wa wakazi wa Kahama aliyejitokeza kupima.
Dk.Kika akiwapima wakazi wa Kahama  Kisukari kwenye  kambi ya Upimaji Bure wilayani Kahama.
Dk. Duma wa NSSF akipima uzito na urefu watu waliojitokeza kupima afya zao.
Wakazi wa Kahama wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha ili waweze kupima afya zao.
Wakazi wa kahama wakiwa kwenye foleni ya kwenda kumuona Daktari.
Wakazi wa Kahama wakisubiria kwenda kuwaona madaktari wanaoendesha zoezi la upimaji Bure.
Dk. Lucy  Simbila akishuhudia Dk. Ali Mzige akimpima Shinikizo la Damu Dk.Charles Rweikiza kuashiria kuanza kwa kambi ya upimaji Afya.
Bw. Kika akipima sukari baadhi ya watu waliofika kwenye zoezi la upimaji Afya bure.
Madaktari wakiwapa ushauri watu waliofika kupima afya zao.
Katikati Afisa uhusiano wa NSSF Jumanne Mbepo akimkabidhi fulana mmoja wa watu waliopima afya.
Wakazi wa shinyanga wakisubiri kwenda pima.

Na Mwandishi Wetu
Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linaendesha  kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Zoezi ambalo lilianzia mkoa wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 ambao watu waliopima VVU ni 1380, linaendelea mkoa wa Shinyanga , Wilaya ya Kahama, kwenye Viwanja vya Barcelona, kuanzia tarehe 04/06/2014, 

 kwa siku mbili mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;
·         Upimaji wa Shinikizo la damu
·         Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
·         Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
·         Utoaji wa dawa za Minyoo
·         Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
·         Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
·         Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Posted by MROKI On Thursday, June 05, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo