Mmililiki wa Makampuni ya Lake Oil Ally Edha Awadh, wazalishaji
wa Gesi ya Lage Gas akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mmililiki wa Makampuni ya Lake Oil Ally Edha Awadh, wazalishaji
wa Gesi ya Lage Gas, akimkabidhi mtungi mpya wa gesi Kamishna Msaidizi wa
Nishati, Norbert Kahyoza wakati wa uzinduzi wa mitungi hiyo jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shaa akitumbuiza katika uzinduzi huo.
Mwongozaji wa shughuli hiyo, Baby Kabaye akiwajibika.
*******
Moja ya makampuni
yanayokuwa kwa kasi, Lake Gas Ltd
Inayojihusisha na usambazaji wa gas kwa matumizi ya nyumbani kuzindua Mitungi ya aina yake tar 18 juni
2014.
Mitungi ya gesi
iliyotengenezwa kwa chuma imekuwa maarufu nchini Tanzania, lakini sasa imefikia
wakati wa mtumiaji kuamua ni aina ipi ya mtungi iliyobora zaidi kwa matumizi ya
familia yake.
“Miongoni mwa sifa za kipekee za mitumngi hiyo ya Lake Gas
ni; mwepesi na yenye kuonyesha kiwango chagesi iliyobakia, hailipuki,isiyo
sababisha uharibifu wa mazingira husika.
Hizo ni sifa ambazo zitamfanya mtumiaji afurahie mitungi hiyo mbali na
muonekano wake unaovutia”. Amesema Ally Edha Awadh mmiliki wa kampuni ya Lake Gas
Mtungi wa kwanza kutoka LakeGas umekabidhiwa kwa mwakilishi
wa Waziri wa nishati na Madini Muheshimiwa Sospeter Muhongo, kamishna msaidizi
wa Nishati Injinia Norbert Kahyoza. Mtunngi huo umekabidhiwa na Ally Edha Awadh
mmiliki wa kampuni ya Lake
Gas.
“Lake Gas wameonyesha njia kwa kuzindua mitungi hiyo bora ya
kipekee, sisi kama wizara tunapongeza jitihada
sio tuu katika kuhimiza upinzani wa kibiashara lakini pia kutoa nafasi za
ajira, na la muhimu zaidi kuongeza pato katika uchumi wa taifa” alisema injinia
Kahyoza.
Mitungi hiyo ya Lake gas imetengenezwa na kampuni iliyobobea
katika utengenezaji wa mitungi ya gesi nchini India
na sasa inapatikana katika ofisi za mawakala wa Lake Gas Dar
es Salaam na Tanzania
kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment