Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa
wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa
shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es
salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka
shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi wametunukiwa vyeti na
zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Afisa Elimu
wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Raymond Mapunda akiongea na wadau mbalimbali wa
elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki
wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es
salaam leo.
Baadhi ya
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es salaam waliohudhuria
hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar Es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali
yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi,
wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio na ushindi
wa mkoa wa Dar es salaam katika mitihani ya taifa ya shule za Msingi na
Sekondari kwa mwaka 2013 leo jijini Dar
es salaam wakati wa hafla ya Siku ya Elimu.
Mkurugenzi
wa Shule ya shule ya Sekondari ya Tusiime ya jijini Dar es salaam Bw. Albert
Katagira akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.
Raymond Mushi (kulia) kufuatia shule yake kutoa wanafunzi bora katika ufaulu wa
masomo katika mitihani ya taifa kwa ngazi ya taifa na mkoa wa Dar es salaam kwa
shule binafsi.
Mwalimu
Stella Kasheba (kulia) kutoka shule ya Sekondari Zanaki akipokea cheti cha
ushindi kwa niaba ya Mkuu wa shule hiyo kufuatia shule ya Sekondari Zanaki ya
jijini Dar es salaam kutoa mshindi Bora wa Jumla kwa shule za sekondari za
serikali katika mitihani ya taifa kwa mwaka 2013
Mwanafunzi
Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akipokea cheti cha pongezi kwa
kuwa mshindi Bora wa jumla katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za
Binafsi za jiji la Dar es salaam.
Mwanafunzi
Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akionesha cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa
jumla kwa wavulana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi
za jiji la Dar es salaam alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond
Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi
Joyce Lymo wa Shule ya Sekondari Kanosa, Kinondoni akionesha cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa
jumla kwa wasichana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 alichokabidhiwa na
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini
Dar es salaam.
Wadau wa
elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa
shule binafsi na viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa
hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar es salaam leo.
safi sana. Hafla imefana sana wanafunzi wajitumekusoma ili mwaka 2014 ufaulu uwe wa kiwango cha juu.
ReplyDelete