Na Father Kidevu Blog
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin kufuatia kufanya vizuri hivi karibuni
katika onyesho kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum
kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria, huku asilimia
kubwa kwenye jukwaa hilo akitumia vazi lililonakshiwa alama za bendela ya Tanzania, ‘National
colours Asia idarous's design’ tayari watu mbalimbali duniani wameombwa
kutengenezewa mtundo huo.
Akizungumza jiini Dar
es Salaam, na mtandao huu, Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak
Fashions, alisema kuwa watanzania na raia mbalimbali wa kigeni duniani kote wametoa order za kutengenezewa
vazi kama hilo ambalo kwa asilimia kubwa limekuwa ni kivutio huku likimweka mtu
yoyote katika hali ya ubora na kupendeza.
Vazi hilo ambalo linabamba ikiwemo aina ya kitambaa maalum
na skafu kubwa inayopachikwa kifuani yenye nakshi ya alam za Taifa, pia tokea
kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye televisheni nchini Nigeria na
Ulala, imekua gumzo kubwa kwa sasa huku wengine wakishahuri liingizwe kwenye
tukio la kusaka vazi la Taifa.
“Kwa sasa nipo katika kushughulikia oda za wateja wangu ambao wengi wapo Mataifa
ya kigeni ikiwemo Nigeria, Ghana, Kenya, uingereza, Marekani na kwingineko
pamoja na Tanzania” alisema Aisa Idarous.
Alisema kuwa, vazi hilo ambalo pia siku ya onyesho hilo
karibu wageni wote wakiwemo balozi wan chi zaidi ya 61 zilizohudhulia siu hiyo
ya Muungano nchini Nigeria, zilivutiwa na hata kulipongeza kutokana na ua
kielelezo cha Utaifa la Tanzania.
Aidha, Asia Idarous alisema kuwa, matilio ya vazi hilo yapo
yanayotoka nchini Tanzania namengine nje ya nchi ikiwemo Nigeria, tayari baadhi hoda zimekamilika na baadhi ameanza
kuziuza katika duka la Fabak fashions lililopo Mikocheni mkabara na Kwa Mwalimu Nyerere.
“Hii ni heshima
kwangu na kwa Tanzania, kwani vazi hili
limeokea kukubalika duniani kote na kupelekea kuwa utambulisho maalum wa
Mtanzania. Vazi hili kwa kawaida anavaa
mtu yoyote na kwenye tukio lolote lile na hata kumweka mtu katika hali ya
umaridadi, ikiwemo kwa wanaume na
wanawake” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous pia aliwataka kwa watu watakao taka kuagiza ama
kutoa order, wanaweza kumpigia +255713263363,
ama dukani kwake Fabak fashions
Mikocheni kwa Mwl.
Nyerere.
0 comments:
Post a Comment