Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) leo Jumanne, tarehe, 20/05/2014 anatarajiwa
kuwasilisha Bajetiya Wizara ya Ujenzi bungeni kwa mwaka 2014/15.
Bajeti hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa jioni, inayosubiriwa
kwa hamu kubwa na wadau pamoja na wananchi inatarajiwa kufafanua mambo
mbalimbali kuhusu sekta hiyo ya ujenzi.
Wizara ya Ujenzi ina majukumu yafuatayo, Kusimamia Sera za ujenzi na usalama barabarani, Ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na
vivuko.
Pamoja na majukumu hayo Wizara pia inasimamia ukarabati
wa majengo ya Serikali, huduma za Ufundi na umeme, kusimamia shughuli za usajili
wa Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Usalama barabarani
na mazingira katika sekta hiyo.
Pia Wizara inasimamia uboreshaji, utendaji na
uendelezaji wa watumishi wa Wizara pamoja na kusimamia utekelezaji wa majukumu
ya Wakala,Taasisi na Bodi zilizo chini ya Wizara.
Kwa taarifa zaidi usikose kusoma toleo la bajeti
ya Wizara ya Ujenzi Kwenye tovuti ya Wizara (www.mow.go.tz) na siku ya alhamisi
tarehe 22/05/2014, kwenye magazeti mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment