Mbunge MO akilakiwa na mmoja wa bibi kizee aliyefika kwenye mkutano wake , Karibu mjukuu wangu hapa Uhamaka.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akiweka saini kwenye kitabu cha ofisi ya kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakati akiwa kwenye ziara ya kiazi ya siku moja kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo, kulia ni diwani wa kata hiyo na Shaban Kiranga. Kushoto ni mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hassan Mazala.
Diwani wa Kata ya Uhamaka CCM, Kiranga akimkaribisha Mbunge MO, Katani kwake kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili sekondari ya Kata hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Uhamaka akisoma taarifa ya ujenzi huo.
Mbunge Dewji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uhamaka wakati wa mkutano wake wa kutembelea jimbo hilo.
Sehemu ya umati wa Kinamama na watoto wa kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakimsikiliza Mbunge wao.
Kikundi cha Ngoma na Kwaya ya kijiji cha Uhamaka wakiimba wimbo wa kumkaribisha Mbunge wao Mohammmed Dewji (MO).
Mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akizungumza kwenye mkutano huo.
: MO akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ya Uhamaka.
Sheikh wa msikiti wa kijiji cha Ititi akimkaribisha MO.
Sehemu ya Msikiti wa kijiji cha Ititi ambapo MO aliguswa na kuwachangia mifuko 30 ya Saruji na Mabati 30 kwa ajili ya kuedeleza ujenzi wao.
MO akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu.
Viongozi wa kijiji cha Uhamaka wakiwa ofisini kwao na Mbunge MO .
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ititi, Jumanne Ivanga akisoma taarifa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ititi kwa Mbunge MO.
MO akihutubia wananchi wa kijiji cha Ititi, pia aliahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.
“ Kwa hiyo mimi kama Mbunge wenu nitatoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu sawa jamani.” Alisisitiza MO huku akishangiliwa na wananchi hao.
Kinamama wa kijiji cha Uhamaka wakimshangilia Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho jana.
Sehemu ya viongozi wa dini na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ititi wakimsikiliza mbunge wao.
Muonekano wa sehemu ya Zahanati ya Kijiji cha Ititi itakapojengwa.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akisalimiana na viongozi wa kijiji cha Unyianga mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara jimbo kwake.
MO akicheza na baadhi ya wanakikundi wa uhamasishaji kwenye hafla hiyo.
MO akisikiliza mashairi kutoka kwa kijana Masoud Mkari mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara jimbo kwake.
Baadhi ya wanakijiji wa Unyianga wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akiwahamisha wananchi kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo.
Mh. Mohammed Dewji akipata picha ya pamoja na wapiga kura wake.
Mh. Mohammed Dewji akikagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara ya jimboni kwake.
Mh. Mohammed Dewji, akifurahi na watoto walipomwambia wanampenda sana wangetamani kuwa kama yeye.
0 comments:
Post a Comment