Baadhi ya wanyange watakao shiriki shindano la Miss Mbagala 2014 wakipozi kwa picha. Waremboi hao Kutoka kulia ni Farida Dimoso, Ester Mnahi na Amina Salim.
Afisa Habari wa Kampuni ya PR Promotion, waandaji wa Shindano la Miss Mbagala, Victor Mkumbo akizunguimza na waandishi juu ya shindano hilo leo. Pamoja nae ni warambo watakao shiriki Miss Mbagala 2014.
********
Na Father Kidevu Blog
KWA mara ya kwanza katika historia ya Mashindano
ya Urembo nchini yatafanyika shindano la Miss Mbagala 2014 ambapo mshindi
ataingia moja kwa moja katika Kandfa ya Temeke na baade Miss Tanzania.
Shindano la Miss Mbagala 2014 ikiwa ni kitongoji
kipya kwa Ukanda wa Temeke linaandaliwa na kampuni ya PR Promotion
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaji
kupitia Afisa Habari, Victor Mkumbo na kusema kuwa shindano hilo litazinduliwa
rasmi ndani ya ukumbi wa nyumbani Mbagala, DAR LIVE usiku wa Mei 9 mwaka huu.
Mkumbo ameiambia Father Kidevu Blog, kuwa jumla
ya warembo 16 wanataraji kushiriki shindano hilo kwa mwaka huu.
Amewataja walimbwende hao kuwa ni Amina Salim (20),
Aquilina Paul (22), Restuta Charles (21), Suzan Paul (19), Natalia Rogath (22),
Grace John (20), Neema Roman (19), Joyce Mkandila (20) na Lulu Baraka (22).
Pia wamo Lucrecia Mushi (20), Subira Ally (23),
Lucy Lyombo (20),Macklina Robert (21), Sylivia Robert (24), Esther Mnahi (20),
na Maureen Msangi (20).
“Hii ni mara ya kwanza kitongoji cha Mbagala
kuandaa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kuongezwa na kamati ya Redds Miss
Tanzania mwaka huu hivyo wilaya ya Temeke itakuwa na vitongoji vinne ambavyo ni
Changombe, Kurasini, Kigamboni na Mbagala” alisema Mkumbo.
Aidha Mratibu wa shindano hilo, Tesha Japhet
amesema bado milango ipo wazi kwa wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini
mahindano hayo na kuleta ufanisi zaidi.
0 comments:
Post a Comment