Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu kata ya Butu Wilayani Igunga Bw Christopher Makoye wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu kwa wananchi wanaounganishwa na kuptia daraja hilo, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora, Manyara na Singida akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Ujenzi wa daraja hilo unagharimu jumla ya shilingi Bilioni 13 za Tanzania linatarajiwa kukamilika hivi karibuni,Wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw. Hassan wa Kasubi.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati aishiriki katika ujenzi wa daraja hilo. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa ujenzi wa daraja la mto Mbutu Bw. Christopher Makoye wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo. Mafundi wakienelea na ujenzi Mafundi wakiwa kazini Moja ya eneo la daraja hilo lilikwa limesukwa nondo. Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw. Elibariki Kingu akizungumza na vyombo vya habari katika eneo hilo la ujenzi mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua ujenzi wa daraja hilo.
0 comments:
Post a Comment