Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2014

Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wapatao 16 tu ndio watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2014 ambalo limepangwa kufanyika Juni 6 katika ukumbi wa Da’ West Park.
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wamepatikana baada ya kufanya mchujo iliyojumuisha warembo 40.
 
Kapinga aliwataja warembo watakaoshiriki kuwa ni Esther Frank Kiwambo (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
 
Wenine ni Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ambasia Lucy Mally (22), Angle Kashaga (22), Faudhia Hamisi Feka (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) , Marry Henry (22) na Mariam Shwaib Hussein (19).
 
Warembo  hao watachuana vikali kutaka kumrithi Dorice Mollel ambaye anashikilia taji hilo. Dorice pia ndiye anayeshikilia taji la Miss Ilala.
Kapinga alisema kuwa warembo hao kujifua kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park chini ya waalimu Neema Mchaki na Pasilida Mandali.
 
Mratibu huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na aina mbali mbali ya burudani ikiwemo wasanii kutoka nje ya nchi. 
 
Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
 
Miss Tabata inadhaminiwa na Zanzi, Redds, Freddito Entertainment, CXC Africa, Father Kidevu Blog, Saluti5, Brake Point na Integrated Communications.
 
Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.
Posted by MROKI On Friday, May 23, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo