Msemaji Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger',
iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi
karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza
utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
******************
Na
Sufianimafoto
wizara
ya fedha imeeleza wazi kuhusu mipango yake ya kutekeleza matokeo makubwa
sasa(BRN) ikiwa ni utraatibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na
kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo
makubwa kwa muda mfupi
Akieleza malengo hayo hayo
msemaji mkuu wa wizara ya fedha, INGIAHEDI MDUMA amesema wizara ya fedha
imejipanga Kutafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi
kufikia mwaka 2015/16
Pamoja
na hayo Mduma amesema pia wamedhamiria kupunguza nakisi katika bajeti ya
Serikali kwa shilingi trilioni 4 kufikia mwaka 2015/16 na Kutekeleza miradi ya
PPP yenye thamani ya shilingi trilioni 6 kufikia mwaka 2015/16
Malengo mengine ni kuhakikisha
kwamba shughuli za BRN zinapatiwa fedha za kutekeleza miradi iliyopangwa ili
kuweza kusimamia malengo yaliyokusudiwa .
Aidha amesema viashiria vya
utafutaji wa mapato vinavyotekelezwa na Wizara ya Fedha vimegawanyika katika
sehemu kuu nne ikiwemo ya mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, ubia katika
sekta ya umma na sekta binafsi na kudhibiti matumizi ya serikali.
katika
kuelezea malengo hayo amesema Katika kipindi cha Julai – Disemba, 2013 jumla ya
shilingi bilioni 215.0 zimekusanywa kutokana na hatua mpya za kodi
zilizoibuliwa kwenye maabara za BRN.
0 comments:
Post a Comment