Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo
ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji nchini Tanzania
katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni pamoja na madini
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe.
Philip Marmo akifungua kongamano hilo
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wajumbe
anayewakilisha wafanyabiashara kabla ya kufungua kongamano la mafuta na gesi linaloendelea huko
Ujerumani kama moja ya maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC) Bi Venosa Ngowi (kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na
shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani. Pembeni ya Waziri ni Balozi wa Tanzania
nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo
Mtaalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST)
Bi. Augustina Rutaihwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (katikati) juu ya
shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania
nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo
Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania
kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa kongamano hilo
0 comments:
Post a Comment