Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakifanya mazoezi katika uwanja wa Sam Nujoma mjini Windhoek Namibia jana. Leo watashuka katika dimba hilo kuwakabili wenzao wa Namibia Brave Warriors katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hafidh Badru akizungumza na wachezaji wakati wa mazoezi.
Nahodha wa Taifa Stars, Agrey Moris akiongoza mazoezi.
*****
TIMU ya taifa Taifa Stars usiku wa leo majira ya saa 2:30 saa za Namibia, itashuka kuwakabili Brave Warriors ya Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha wa mpito, Salum Madadi na Hafidh Badru kutoka Zanzibar kitawakosa nyota wake watatu wanaosakata soka la kulipwa nje ya Tanzania.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha wa mpito, Salum Madadi na Hafidh Badru kutoka Zanzibar kitawakosa nyota wake watatu wanaosakata soka la kulipwa nje ya Tanzania.
Nyota hao ni Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wanakipiga TP Mazembe ya Congo DRC na kiungo
Mwinyi Kazimoto anaekipiga Al Markhiya timu iliyopo daraja la pili mji wa
Qatari.
Baada ya mazoezi ya
leo usiku katika uwanja wa Sam Nujoma, Kocha Madadi anataraji kupata kikosi cha
kwanza ambachjo kitatokana na wachezaji 15 aliowasili nao jana hapa Namibia
tayari kukivaa kikosi cha wachezaji wa Brave Warriors ambacho kinadaiwa
kuwa na majeruhi 3.
Madadi ambaye ni
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, ataunda kikosi cha kwanza kutoka kwa
wachezaji Shaban Kado, Mwadin Ally, Erasto Nyoni, Abdi Hassani Banda, nahodha
Agrey Moris na Said Morad.
Wengine wanaotaraji
kuunda kikosi hicho ni Himid Mao, Amri Kiemba, Ramadhani Singano, Haruna
Chanongo, Athanas Mdamu, Juma Luizio, Jonas Mkude na Mcha Khamis Mcha.
Msafara wa timu ya
taifa unaoongozwa na Mjumbe wa Kanda ya Simiyu na Shinyanga, Epaphra Swai
pamoja na kocha msaidizi Hafidh Badru, Mjumbe Ahmed Mgoi, Daktari wa timu Juma
Mwankemwa, Meneja wa timu, Boniface Clemence.
Licha ya kukosa nyota
hao wachezaji wameahidi ushindi mnono katika mchezo huo wa kimataifa na kulinda
hadhi yao katika viwango vya soka vya FIFA.
Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema wao kama wadhamini
wanatarajia ushindi mkubwa ili kuipandisha Tanzania katika viwango vya
FIFA.
Huu ni mwaka wa pili
tangu Kilimanjaro Premium Lager ianze kuidhamini Taifa Stars na imewekeza zaidi
ya Dola Milioni mbili kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment