WAZIRI MKUU Mizengo Pinda aagiza huduma za upimaji wa
figo zitolewe kwa kuzunguka katika kanda zilipo nchini na kuacha utamaduni wa
kutoa huduma hizo wakati wa maadhimisho hayo tuu.
Alisema hayo Jana mchana (Alhamisi, Machi
13, 2014), wakati wa akifunga kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Afya ya Figo
Duniania yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere mkoani Dodoma, yenye kauli
mbiu Figo Huzeeka kama wewe. Jali Afya
ya Figo zako.
Akizungumza na wananchi wakati wa kilele hicho Waziri
Mkuu aliwaeleza wananchi kujenga utamaduni wa kujali na kupima afya zao mara
kwa mara: ‘‘Tumieni fursa hii ya uwepo wa huduma hizi karibu nanyi kujua hali
ya afya ya figo zenu ili mchukue hatua stahiki mapema, kuchelewa kujua afya
yako kunaweza kuathiri pia urahisi wa matibabu kama ukigundulika kwamba
umeathirika na Ugonjwa wa Figo“.
Alisema, huduma kama hizi za Klinic ya Umma yaani Public Clinic zitolewe mara kwa mara
kikanda bila kusubiria maadhimisho ili kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati na
kuendelea kuhamasisha huduma za afya za aina hii kwa wananchi, walau kuweza
kutoa huduma hizi katika Kanda ya juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi
na Kanda ya Kaskazini mtakuwa mmefanya jambo la busara sana kwa watanzania.
Waziri Pinda alisema, zipo njia muhimu za kuzingatia ili
kuepukana na ugonjwa wa figo kama inavyoelezwa na wataalum kuwa ni pamoja na
kufanya mazoezi kwa wingi, kunywa maji glass 6 hadi 8 kila siku, kuacha kuvuta
sigara, kuzingatia uzito wa mwili na kuacha kutumia dawa kabla ya maelekezo ya
daktari, aliongezea Waziri Pinda.
Waziri Mkuu alisema, ‘‘Dawa hapa ni Kinga na Sio Tiba“
hivyo aliwaomba wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili
kuweza kufahamu na kupunguza madhara makubwa ya ugonjwa huu.
Changamoto kubwa iliyopo mbele yetu kama serikali ni
upungufu wa madaktari bingwa wa kutosha wa kutibu magonjwa ya figo, kupandikiza
figo na gharama kubwa za matibabu ya figo ambayo huduma hiyo haipatikani hapa
nchi hivyo: ‘‘Serikali itachukua jukumu la kuongeza idadi ya wataalamu wa figo na
kwa kuzingatia suala hili tutaliweka katika bajeti ya Serikali ya mwaka“,
alisema Waziri Mkuu.
Alieendelea kusema kuwa, kuna Sera ya Magonjwa ya Afya ya
mwaka 2007,Miongozo na Mikakati ya kupambana na ugonjwa huu hivyo, Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Figo Tanzania,
itazindua ripoti ya Wiki ya Afya ya Figo 2013 Tanzania, ambapo ripoti hiyo
itaonesha kuwa watu 4,325 walijitokeza kupima afya za figo zao na kati ya hao
asilimia 15 (623/325) walipatikana na matatizo ya figo. Ni dhahiri kuwa, juhudi
hizi za kubaini ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa Figo, zinazofanywa na Serikali
zitarahisisha na kuwezesha wananchi wengi kupata taarifa mbalimbali kutoka
ndani na nje ya Nchi kuhusu afya ya figo.
Pamoja na kuhudhuria Kilele cha maadhimisho hayo, Waziri
Mkuu alizindua rasmi tovuti ya Taasisi ya Taifa ya Figo ambayo itakuwa inalezea
masuala yote yanayohusu figo na kusisitiza wananchi kutumia tovuti hiyo
kujifunza masuala yote masuala mbalimbali ya figo.
Mapema, Prof.
Ephata Kaaya, ambaye ni Mjumbe wa Bodi Taasisi ya Taifa ya Figo alieleza kuwa
dira na malengo ya taasisi hiyo ni kuwa kitovu cha taifa katika kuendeleza na
kuthibiti magonjwa ya figo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wingi, kufanya tafiti
mbalimbali ili kuweza kufaham takwimu halisi za ugonjwa huo, kwani katika maadhimisho
haya jumla ya wananchi 3800 wameweza kusajiliwa na wananchi 3120 wamefanyiwa
uchunguzi.
Taasisi
ya Taifa ya Figo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya, Sekta Binafsi na
wananchi kuendesha masuala ya matibabu ya figo na kubuni mbinu mbadala ya
upatikanaji wa fedha ili kuweza kuendesha Taasisi hiyo ambayo hivi sasa inatoa
huduma za matibabu ya figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya
Rufaa Mbeya, na huduma hizo pia zitaanzishwa katika Hospitali za Rufaa Bugando
na KCMC.
0 comments:
Post a Comment