MTANZANIA Jackline Sakilu amewatuliza Watanzania kwa
kuibuka mshindi katika mbio za mwaka huu za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon.
Sakilu ambaye anatokea katika Jeshi la wananchi la Tanzania
(JWTZ), amefanya hivyo jana katika mbio za Kilomita 21 wanawake, akikimbia kwa
muda wa saa 1:12:43 mbele ya wanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya.
Katika nafasi ya pili alikuwa ni mwanariadha Cynthia
Towett, aliyekimbia kwa muda wa saa 1:14:33, na katika nafasi ya tatu alikuwa
ni Naomi Maiyo aliyekimbia kwa muda wa saa 1:17:47 wote kutoka Kenya.
Katika mbio hizo kwa upande wa wanaume, nafasi ya
kwanza alikuwa ni Alfred Lagat kutoka Kenya ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:02:34
akifuatiwa na Wakenya wenzake Silah Limo (1:03:04) na Keneth Kandie (1:03:20)
huku Mtanzania wa pekee katika kumi bora, Alfred Felix, kutoka Klabu ya riadha
ya Holili (HYAC) akishika nafasi ya tano (1:03:27).
Wakati huo huo zimwi la kufanya vibaya katika mbio
ndefu (Kilomita 42) imeendelea kuiandama Tanzania baada ya Wanariadha kutoka
Kenya kutawala mbio hizo kwa mwaka mwengine tena.
Katika Mbio za wanaume, Mshindi wa
kwanza David Ruto kutoka Kenya aliyetimua mbio hizo kwa muda wa masaa 2:16:04,nafasi
ya pili alikuwa ni Julius Kilimo (2:16:17) na nafasi ya tatu ikishikwa na
Victor Serem 2:16:32 huku Mtanzania wa kwanza katika mbio hiozo kwa upende wa
wanaume, Daudi Lwabe, akiingia katika nafasi ya nane akitumia muda wa masaa 2:18:34.
Katika upande wa wanawake mshindi alikuwa ni Frida
Lodera aliyetumia muda wa masaa 2:40:11, nafasi ya pili ni Joan Rotich
aliyetumia muda wa masaa 2:42:46 na nafasi ya tatu ikashikwa na Abigal
Toroitich ambaye alitumia muda wa masaa 2:55:14 ambapo Mtanzania pekee aliyeingia
kumi bora, Banuelia Bryton, akiingia
katika nafasi ya tisa kwa kutumia muda wa masaa 3:12:26.
WATANZANIA WAENDELA
KUFANYA VIBAYA.
Pamoja na waandaaji wa mbio hizo kuendelea kutoa ahdi
nyingi za kuongeza zawadi kwa washindi wazalendo, wanariadha wazawa wameendelea
kufanya vibaya katika mbio hizi.
Katika mbio za mwaka huu, wanariadha kutoka nchi jirani
wameendelea kuonesha umwamba katika riadha hasa mbio ndefu mbeloe ya watanzania
tofauti na ilivyo katika miaka ya 70 enzi za akina Filbert Bayi na Suleiman
Nyambui.
Kutokana na matokeo ya mbio za mwaka huu, nafsi zote za
juu, nafasi ya kwanza hadi ya tano, tofauti na mbio za kilomita 21 kwa upande
wa wanawake uliochukuliwa na Jackline Sakilu, mbio zote zilitawaliwa na wakenya
huku Watanzania wakilazimika kushika za nafasi ya tano, nane na tisa.
WAZIRI MUKANGARA AAGIZA
RT KUANZA MAANDALIZI MAPEMA KUFUTA UTEJA.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dkt. Fenella Mukangara ameitaka cham cha Riadha Tanzania (RT),
kuhakikisha inaweka mikakati mizuri ya kuwaanda wanariadha wanaoshiriki mbio za
kitaifa na kimataifa ili kuwafanya kuwa tayari kuliko kusubiri hadi mashindano yafike
ndipo waanze kufanya maandalizi.
Dkt. MUkangara ambaye aliokuwa mgeni
Rasmi katika mbio za mwaka huu Kilimanjaro marathon, aliyesema hayo katika
hotuba ambapo aliwataka viongozi wa michezo riadha ikiwemo kujiandaa kikamilifu
kushiriki mashindanoi yanayoandaliwa hapa nchini.
Alisema Wadhamini wanatumia fedha nyingi
kuandaa mashindano lakini kutokana na ushiriki mbovu wa watanzania unaochangiwa
na maandalizi duni, umekuwa ukiwakatisha tamaa watu wenye nia ya kuwekeza
katika michezo hapa nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, ambao ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo kwa mwaka wa 12 sasa, George
Kavishe, alisema TBL itaendelea kuhakikisha inaboresha udhamini wake katika
mashindano hayo na kuendelea kuyapa sura ya kimataifa zaidi.
0 comments:
Post a Comment