Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. John Gabriel Tupa (pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime.
Habari
zilizothibitishwa zinasema Marehemu Tupa alianguka na kupoteza fahamu
akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. John Henjewele,
alikokuwa akipokea taarifa kabla ya kufunga mafunzo ya mgambo wilayani
humo.
Mara
baada ya kuanguka juhudi za haraka zilifanyika za kumkimbiza hospitali
ya Wilaya ya Tarime ambako alitangazwa kuwa ameshafariki mara
alipofikishwa hapo.
Mwili wa Marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Mara ili kuhifadhiwa wakati taratibu za m,aziko zikiandaliwa.
Tutaendelea kuwapasha kinachoendelea kwa kadri taarifa zitavyokuwa zikitufikia.
0 comments:
Post a Comment