Mgombea
Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa na wafuasi wa
chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada
kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM)
kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko
kwenye jimbo hilo la Kalenga.
*******
Matokeo
ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi
jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM
kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA
kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia
79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya
jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.
KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA SALIM ASAS AKICHEZA KWA SHANGWE VIWANJA VYA CCM MKOA KUSHEREKEA USHINDI WA CCM KALENGA
Matokeo ya Awali yasiyo rasmi baadhi ya vituo inaongoza kwa mbali.
0 comments:
Post a Comment