Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2014

 Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya milima ya Pare Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro zimeporomosja maj na kusabisha mafuriko katika eneo la Kijiji cha Mgagao na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara kuu ya Moshi - Same mkoani humo. Pichani ni moja ya magari yakielekezwa namna ya kuvuka na vijana wakazi wa eneo la Mgagao ambao hufanya hivyo kwa kulipwa ujira kidogo.
 Mwendesha bodaboda akipita katika dmbwi hilo la maji eneo la Mgagao.
 Gari likipitwa kwa kuongozwa na vijana wa Mgagao.
 Vijana hao wakichukua ujira wao kutoka kwa dereva wagari.
Fedha huleta ugomvi na chuki, pichani vijana hao wakitaka kugombana baada ya kulipwa ujitra wao huo wa kuliongoza gari. Baadhi ya watu wamedai maji hayo huzidi na kyusababisha magari kukwama eneo hilo, hivyo kuiomba serikali kupitia Wizxara ya Ujenzi na TANROADS kuweka daraja au kalavati kubwa eneo hilo kunusuru athari zaidi za maji hayo.
Posted by MROKI On Monday, February 10, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo