Marehemu Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mmoja wa watoto wake kwenye ibada maalum ya kutoa shukrani alipotimiza miaka 100 iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni jijini Dar hivi karibuni.
Familia nzima ya Nkhoma Kambonapany wanasikitika kutangaza kifo cha baba na babu yao mpendwa Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany, kilichotokea kwenye hospitali ya Mount Ukombozi tarehe 17/01/2014.
Taarifa za msiba ziwafikie Doctors Colin na Nicholas Darch wa Cape Town Afrika Kusini , Bi Laura Amrei wa Hamburg Ujerumani , Bi Ajira Darch wa San Fransisco , California , Marekani , Bwana Monday Wamunza akiwa Maryland , Marekani , ndugu na jamaa popote walipo.
Alijaliwa kupata watoto 11, wajukuu 36 , na vitukuu 25. Msiba unafanyika kwa mtoto wake Professor Alice Wamunza Nkhoma , Nyumba na. 07 , Mtaa wa Koroshoni , Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Maziko yatafanyika tarehe leo 19/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni.
Msafara wa mazishi utaanzia saa tano za asubuhi chuo kikuu baada ya chakula na kutoa heshima za mwisho. Baada ya hapo utaelekea Kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni kwa ajili ya Misa.
Baada ya hapo utaelekea Kinondoni makaburini kwa kumpumzisha Mzee Kambonapany.
0 comments:
Post a Comment