Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo juzi Ofisi ndogo ya Bunge Dar es Salaam kujadili fedha za elimu hasa katika manunuzi ya madawati na vitabu vya wanafunzi. Kushoto ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Ismail Aden Rage.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakifuatilia mkutano huo. Kutoka kushoto ni Zainab Vulu, Ezekiah Chibulunje, Lucy Owenya na Catherine Magige.
Catherine Magige (kulia) akijadili jambo na Mbunge na mjumbe mwenzake wa PAC, Lucy Owenya.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Jumanne Sagini (kushoto) akijibu hoja za wajumbe wa PAC kuhusiana na manunuzi ya vitabu mashule kupitia fedha za rada zilizorejeshwa nchini.
Wajumbe wa PAC walitembelea shule ya Msingi Bunge kuthibitisha maelezo ya Katibu Mkuu juu ya manunuzi ya vitabu mashuleni na hapa wanakartibishwa na mwalimu Mkuu wa Bunge, Hadija Telela
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Ismail Rage akiongea na mwalimu wa darasa la saba Kuluthum Kazumari juu ya vitabu.
Wajumbe wa Kamati wakiwa katika moja ya darasa
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akiangalia vitabu hivyo.
Mjumbe wa PAC, Godluck Ole Medeye akimpa zawadi mwanafunzi aliyejibu swali lake vizuri.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akikagua vitabu hivyo. Kulia ni Mwalimu Mkuuwa sule hiyo Hadija Telela.
Mjumbe wa PAC, Zainab Kawawa akiangalia vitabu.
0 comments:
Post a Comment