Kama tulivyotoa taarifa kwa vyombo vya habari hapo
awali wakati wa Sikukuu ya Noel [Christmass ] Redds
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, baada ya kujumuika na watoto waishio
katika mazingira magumu kule Bigwa Morogoro katika Kituo cha Mgolole,
Mrembo huyo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo
Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tatu Clara Bayo, kukabidhi misaada ya kijamii
pamoja na kushereheka nao pamoja wakati wa Sikukuu ya Mwaka mpya tarehe 1
Januari 2014, katika kituo kiitwacho Nira Children and Youth Orphans Foundation
kilichopo eneo la Mbagala Nzasa A, kwa mzungu kaburi moja, Kata ya Charambe,
Wilaya ya Temeke.
Miss Tanzania pamoja na warembo wenzake, watakabidhi misaada
hiyo ya vyakula, ikiwa ni pamoja na vifaa vya shule, kama vile Madaftari,
kalamu, vitabu n.k.
Wakati huo huo Mrembo wa Kanda ya Mashariki Diana Laizer, kutoka Mkoa wa Morogoro, nae
atakabidhi misaada kama hiyo katika Kituo cha Amani kilichopo Manispaa ya
Morogoro, pamaja na kushereheka nao katika Sikukuu hii ya Mwaka mpya 2014.
0 comments:
Post a Comment