Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (aliyeshika kipaza sauti)
akiwaonyesha wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam –Rashid Ahmed
Othman (kati kati) na Peter Elias Magusha (wa pili kutoka kulia), jinsi
mashine inavyochangua namba ya mshindi katika droo ya Mimi ni Bingwa
promotion iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki Mbagala Zakiem na kutangazwa
washindi watano wa wiki hii wa shilingi milioni moja moja. Zaidi ya
shilingi milioni 40 tayari zimetumwa kwa washindi mbali mbali na tiketi
nne kwa washindi wawili wa wiki kwenda kuangalia mechi ya klabu ya
Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa
Old Trafford. Kulia ni Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (aliyeshika kipaza sauti)
akimpigia simu mmoja wa washindi wa Mimi ni Bingwa promotion wakati wa
droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki Mbagala Zakiem Jijini Dar es
Salaam na kutangazwa washindi watano wa wiki hii wa shilingi milioni
moja moja. Zaidi ya shilingi milioni 40 tayari zimetumwa kwa washindi
mbali mbali na tiketi nne kwa washindi wawili wa wiki kwenda kuangalia
mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini
Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford. Kati kati ni mkazi wa Mbagala
jijini Dar es Salaam –Rashid Ahmed Othman akihakiki namba ya mshindi
baada ya kuonyeshwa mashine inavyochangua namba ya mshindi katika droo
hiyo. Kulia ni Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha ya Tanzania.
========== ======== ===========
Airtel yamwaga zawadi ya milioni 40 katika 'Mimi ni Bingwa' promosheni
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Airtel Tanzani imeshazawadia wateja wake zaidi ya
shilingi milioni 40 katika promosheni yake ya 'Mimi ni Bingwa' yenye
lengo la kuwazawadia wateja wake na kuongeza chachu ya mpira wa miguu
nchini.
Hii
ilithibitishwa na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bw.
Jackson Mmbando wakati wa kuangalia mechi ya Ligi kuu ya Uingereza kati
ya klabu ya Manchester United na Newcastle iliyoonyeshwa bure eneo la
Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam.
Alisema
mbali na zawadi ya fedha inayotolewa kwa kutumwa kupitia Airtel Money,
washindi wawili wa tiketi pamoja na safari inayogharamiwa na Airtel
kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) za klabu ya Manchester
United katika uwanja wa Old Trafford, watasaidiwa katika utafutaji wa
hati za kusafiria pamoja na washindi wawili watakaopatikana katika droo
ya wiki ya tatu na nne.
Mmbando
ambae wakati wa tukio pia alitangaza washindi wengine watano wa
shilingi milioni moja kila mmoja wa wiki hii, alisema promosheni
inayotokana na ushirikiano kati ya Manchester United na kampuni hiyo ya
simu hailengi tu kuwazawadia wateja lakini pia kuwaunganisha wateja na
soka la kimataifa hatua ambayo itaongeza chachu ya wapenda michezo
Tanzania.
''Airtel
imeweka vituo mbali mbali ambavyo wapenda soka wataangalia mechi za
klabu ya Manchester United bure kupitia luninga kubwa. Leo tunawaonyesha
wakazi wa Mbagala mechi kati ya Manchester United na Newcastle, lakini
pia tunavituo vingine ambavyo tunaonyesha mechi zote za Man U bure.
Vituo hivi ni kama Mbeya, Shaba Pub Mwanza -Shooters Pub, Dodoma - Four
Ways, Dar es Salaam - Rose Garden, Morogoro - Nyumbani Launge na Arusha -
Empire Sports bar,'' alisema Mmbando.
Mmbando
alisema kuwa bado zawadi nyingi kushindaniwa na kusema kuwa mbali na
shilingi milioni 2 za kila siku, milioni 10 kila wiki na tiketi 2 kwa
watu wawili kila wiki, bado kuna zawadi ya kubwa ya shilingi milioni 50
kushindaniwa mwishoni mwa promosheni. Alisema ili mteja kushiriki kwenye
promosheni, anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) yenye neno "BINGWA"
kwenda namba 15656.
Licha
ya washabiki wa Man U kuvunjika moyo baada ya kufungwa goli moja na
Klabu ya Newcastle United katika mechi iliyochezwa uwanja wa Old
Trafford waliburudishwa na wasanii wa Bongo Flava kama Ney wa Mitego,
Young Killer na Kinoko Comedy Group.
0 comments:
Post a Comment