Nafasi Ya Matangazo

November 13, 2013

Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akitoa maagizo kupitia hotuba yake,wakati wa mkutano wa siku ya wadau wa mfuko wa NHIF/CHF ,kulia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NHIF Charles Kajege .
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Regina Chonjo akipokea tuzo ya kinyago cha umoja kwa kutambau mchango wa viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea katika kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF sanjari na msaada mashuka 30 kwa ajili ya wodi ya akina mama wa hospitali ya wilaya hiyo kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya,anayekabidhi ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila ambaye alikuwa mgeni rasmi,wakati wa kongamano la siku ya wadau wa mfuko huo.
mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Charles Kajege akitoa salamu za bodi na maombi maalum kwa viongozi wa Mkoa,wadau na wanachama wa NHIF/CHF wakati wa kongamano la siku ya wadau wa mfuko huo uliofanyika Mkoani Lindi,kushoto mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Hamid Nassoro,kulia Mkurugenzi wa rasilimali Watu na Utawala Beatusi Chijumba,na Fortunata Raymond msimamizi wa mfuko ofisi ya Lindi.
Wadau wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila wakati wa kongamano la siku ya wadau wa NHIF wa Mkoa wa Lindi,uliofanyika mkoani humo kwenye ukumbi wa kagwa.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NHIF Charles Kajege akikagua kifaa tiba (Ultra Sound) kilichotolewa kwa mkopo kwa wa thamani ya 54milioni kwa hospitali ya mkoa wa Lindi,mfuko umekuwa ukitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya riba nafuu na ukarabati wa majengo hili kuboresha huduma za matibabu hususani vijijini,kulia ni afisa udhibiti ubora wa mfuko Dr. Beatrice Mwakipesile.
Posted by MROKI On Wednesday, November 13, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo