James
Rugemarila akiwaonesha waandishi wa habari Windhoek feki ya chupa
ambayo imeingizwa kinyemela na watu wanaoihujumu kampuni hiyo. Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benedictor Rugemarila akiwaonyesha waandishi
wa habari Windhoek halisi inayosambazwa na kampuni ya Mabibo.
Habari, Picha na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es Salaam
********
Kampuni
ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD ya jijini Dar es Salaam, yenye
kibali cha kuingiza na kusambaza bia zenye nembo ya Windhoek imewataka
watu wote wenye Windhoek Beer zisizo na Nembo ya MB66 kuzisalimisha
wenyewe kwa hiari polisi vinginevyo watashitakiwa kwa makosa ya wizi wa
mali ya Mabibo na kutotii amri ya mahakama.
Mshauri
wa Biashara wa Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer, James Rugemarila
akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye mkutano alioutisha
ofisini kwake alisema kuwa, kwa mujibu wa mkataba “ Registerered User
Agreement” kati ya Namibia Breweries Limited ambao ni watengenezaji wa
bia zenye nembo ya “Windhoek” na Mabibo Beer Wines and Spiritis Limited,
mkataba ambao umesajiliwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na
Huduma (Trade andi Service Marks ACT, Cap. 386 of the Laws of Tanzania
R.E. 2002) Mabibo ndiyo Muingizaji na Msambazaji pekee wa bia zenye
nembo ya Windhoek na hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuingiza na
kusambaza bia zenye nembo ya Windhoek bila kibali cha Mabibo.
Rugemarila
alisema ili vinywaji vinavyozasambazwa na kampuni yake kutambulika
vyema na wanywaji imechapisha jina la Mabibo Beer Wines and Spirits LTD
kwenye kasha na kwenye chupa zenye MB66.
“Tumefanya
hivyo ili kurahisisha utambuzi wa Windhoek kwa wateja wetu kuepuka
udanganyifu unaofanywa na wafanya biashara wanaotuhujumu,” alisema
Rugemarila.
Akifafanua
kuhusu biashara ya Windhoek MB66 alisema kuwa ina faida ya Shilingi
14,000 kwa katoni, akaongeza kuwa mlaji wa Windhoek akiuziwa chupa moja
bei ya shilingi 3,000/= kwa chupa, muuzaji anapata faida ya 14,000 kwa
katoni ambayo ni kubwa zaidi kuliko faida ya bia zingine kwenye soko la
bia Tanzania.
Mshauri
huyo alisema, Mabibo Beer imeamua kuvipelekea vinywaji vyake vyombo vya
usalama nchini kwa vile inatambua umuhimu wake ambapo wanausalama hao
watakuwa wakiuziwa Windhoek ya kopo.
“Windhoek
bia ya kwenye makopo itakuwa kwa ajili ya matumizi ya Maafisa na askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza
na familia zao kwa sababu hazitozwi kodi,” alisema Rugemarila.
Rugemarila
aliongeza kuwa, kuanzia sasa Jeshi la Polisi litazikamata Winhoek za
wizi na magendo zitakazokutwa zikiuzwa mitaani na wahusika watashtakiwa
kwa kosa la kufanya biashara kinyume cha sheria.
Aidha, aliwakaribisha watu wanaohitaji kufanya biashara ya Windhoek kwa njia ya halali ambapo alisema wawasiliane na idara ya masoko au uongozi wa Mabibo Beer Wines and Spirits LTD.
Ruggemarila
alitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said
Mwema, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Mkoa wa Kipolisi wa Dar es
Salaam, Suleiman Kova, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Egilbert Kiondo
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kwa ushirikiano
inayowapa.
Vinywaji
vinginne vinavyosambazwa na Kampuni ya Mabibo Beer ni Climax Non
Alcoholic Herbal Energy Drink kinywaji ambacho hakina kilevi, kinaongeza
nguvu na hutengenezwa kutokana na mimea asili.
Kuhakikisha
kinywaji hicho kinatambulika nchi nzima, Rugemarila alisema Mabibo Beer
itafanya promosheni ya Windhoek sehemu mbalimbali kuanzia sasa hadi
Desemba 2013.
Hivi
karibuni, Kampuni ya Mabibo ilifungua kesi katika mahakama ya Kisutu
dhidi ya wafanyabiashara wawili, Ambele Mwasyeba na Sebastian Kavishe
wanaoiujumu kampuni hiyo. Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani
Septemba 25, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment