Washindi wa shindano la Biggest
Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na Mwenzake Mark wakitembezwa na
kuangalia namna walemavu wa kituo cha Shanga
River House cha jijini Arusha, washindi hao waliopatikana kupitia kampuni ya
My Destination walikuwa nchini na kutembelea vivituo mbalimbali vya utalii na
kukagua miradi mbalimbali kama hiyo.
Mshindi wa shindano la Biggest
Baddiest Bascket, Allex Ayling akipuliza
kioo kilicho yeyushwa tayari kwa
kutengenezwa chombo chochote ambavyo hutokana na taka ngumu zinazozalishwa na
binadamu ikiwa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha
shanga river house cha jijini Arusha.
Allex na Mark wakipewa maelezo ya shughuli za kituo.
WADAU mbalimbali wa
utalii wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuutangaza utalii wa Tanzania katika
maeneo yao ili kuwavutia watalii wengine kuzidi kufika kwa wingi hapa nchini
kujionea maliasili zilizopo na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
Hayo yalielezwa jana na
Afisa Mtendaji wa TATO ,Sirili Akko wakati akizungumza na wadau wa
maswala ya utalii waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza vijana wawili
walioshinda shindano lililoandaliwa na kampuni ya My Destination
lililoshirikisha washiriki 122 ulimwenguni.
Aidha alisema kuwa
,Tanzania ni nchi ambayo imebahatika kupata vivutio mbalimbali vya utalii hivyo
kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili zetu, hivyo hawana budi
kuutangaza utalii wetu katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa
nchi za Afrika.
Alisema kuwa, shindano
hilo lilihusu mshiriki kuchagua vitu ambavyo wangependa kufanya maishani kabla
hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki katika shindano hilo na
kuoanisha kuwa wao wangependa kutembea dunia nzima na kujionea maajabu yaliyopo
katika vituo mbalimbali.
‘baada ya vijana hao
kushiriki shindano hilo walishinda na kupewa nafasi ya kuchagua
kutembelea nchi 25 kati ya 80 ambazo katika hizo nchi 25 walichagua nchi tatu
za Afrika ikiwemo kutembelea Tanzania,Zimbabwe,na Afrika ya kusini na ndo maana
wapo hapa leo tayari kwa kuanza zoezi hilo’alisema Akko.
Aliongeza kuwa, kitendo
cha wao kuchagua Tanzania kati ya nchi 25 kimewafariji sana wao kama
wadau wa utalii kwani imeonyesha jinsi ambavyo utalii wa nchi yetu unaweza
kutangazwa na watalii mbalimbali na hatimaye kuweza kupata wageni wengi zaidi
kwa kujionea maliasili zilizopo katika maeneo yetu.
Nao vijana hao
walioshinda shindano hilo kutoka Calfonia Alex Ayling na Mark Ayling
walisema kuwa, shindano hilo waliweza kushinda baada ya kukithi viwango
vya shindano hilo na hatimaye wamefurahia sana kushinda kwani mchuano
uliwashirikisha watu mbalimbali ulimwenguni.
Alex alisema kuwa, lengo
la kuchagua Tanzania miongoni mwa nchi tatu za Afrika ambazo wangependa kutembelea
ni kutokana na uoto wa asili uliopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya
Serengeti kwa ajili ya kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao
.
Alisema kuwa,katika
maeneo hayo yote watakayotembelea watakuwa wakichukua mikanda mbalimbali kwa
ajili ya kuirusha kwenye mtandao na hatimaye watu mbalimbali kuweza kujionea
vivutio mbalimbali vilivyopo katika vituo watakavyotembelea.
Mark alisema kuwa,
wamekuwa wakifuatilia vitu mbalimbali vinavyoendelea Tanzania ikiwemo wanyama
mbalimbali wa kuvutia , pamoja na kufuatilia makabila ya wamasai ambayo
watakuwa na nafasi ya kuwatembelea na kuweza kujifunza maswala mbalimbali
kutoka kwao.
walipewa zawadi na marafiki mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment