KAMPUNI ya Vodacom leo imewapiga jeki vifaa vya michezo Jukwaa la Wahariri (TEF) na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), ambao wanatarajia kupambana jumamosi ijayo mkoani Iringa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa TEF.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salim Mwalimu alisema wametoa vifaa hivyo kutokana na kuthamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari pamoja na uhusiano mzuri waliokuwa nao.
“Kila mwaka hufanya mikutano yao, tumeona tuungane nao kupitia mechi yao hiyo, ambayo itawaondolea uchovu waliokuwa nao mara baada ya kumalizika mkutano wao huo, ambao ni mara ya tatu kufanyika, pia itazidi kuboresha mahusiano yetu ya muda mrefu,” alisema Mwalimu
Vodacom imetoa seti tatu za jezi, mbili kwa timu hizo, huku ya tatu atapewa bingwa atakayeibuka na ubingwa kwenye mechi hiyo, pia imetoa mipira sita, ‘track suit’ nne pamoja na viatu seti mbili, vifaa vyote hivyo vina thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 3.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, nahodha wa timu ya TEF, Kulwa Karedia aliishukuru kampuni hiyo na kuahidi wataifunga timu hiyo ya Iringa na kurudi na zawadi ya seti moja ya jezi pamoja na mpira.
0 comments:
Post a Comment