Swala kuu ya Eid El Haj imeswaliwa katika Msikiti wa Al-Farouk (BAKWATA) Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi katika swala hiyo ni Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe (MB), pichani ni waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala hiyo msikitini hapo leo asubuhi.
Swala kuu ya Eid El Haj imeswaliwa katika Msikiti wa Al-Farouk
(BAKWATA) Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi katika swala
hiyo ni Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe (MB), pichani ni waumini wa
Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala hiyo msikitini hapo leo asubuhi.
Mgeni rasmi katika Swala ya ya Eid El Haj, Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe (MB),(wanne kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Msikiti, Dini ya Kiislamu, na serikali katika Swala kuu ya Eid El Haj katika Msikiti wa Al-Farouk
(BAKWATA) Kinondoni jijini Dar es Salaam msikitini hapo leo asubuhi.
Utoaji wa Zakaah ni nguzo ya tatu kati ya nguzo tano za dini ya Kislamu hivyo watoto kama hawa hawana budi kufundishwa na kuongozwa katika utoaji Zakaah namna hii. Nguzo nyingine za Uslamu ni pamoja na Shahada ya Imani, Swalah,Kufunga katika Mwezi wa Ramadhaan Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhaan na Kuhiji Makkah
Waumini wakisikiliza baraza la Eid.
Wakina mama wakusanya zaka wakipita....
Muumini wa dini ya Kiislamu, Rehani Athuman akimchukua Binti yake baada ya swala hiyo msikitini hapo.
Mtoto huyu nae alihudhuria Swala hiyo.
Mmoja wa waumini wa Dini ya Kiislamu walio hudhuria Swala hiyo ya Eid El Haj msikitini hapo akitoka.
0 comments:
Post a Comment