Nafasi Ya Matangazo

October 02, 2013

Makamu wa Rais wa International Association of  Public Health Institutes(IANPHI)ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(Nimr)Dk Mwelecele Malecela akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Ngurdoto,Arusha baada ya kufungwa Mkutano wa Nane wa IANPHI ambao umekua na mafanikio makubwa.
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Mkutano wa kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa cha afya za Jamii(IANPHI),umefungwa jana jioni na kuwapa fursa wageni hao kutoka nchi 35 ulimwenguni kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujionea vivutio mbalimbali.

Mkutano huo ulianza Septemba 29 hadi Oktoba 1,2013 katika hoteli ya kitalii ya Ngurdoto huku mada mbalimbali zikitolewa na kuwapa uelewa mkubwa washiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Dk Mwele Malecela amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na umuhimu wa taasisi za afya ya jamii katika mataifa mbalimbali.Ambao umejadili namna ya kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na magonjwa yanayoambukizwa kutokomezwa.

"Tumejadili kwa kina kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni tatizo kubwa katika mataifa mengi hasa Afrika na kuona wenzetu wamefanikiwa kwa kiwango gani kukabiliana nayo,tumepata uzoefu kutoka kwa wataalamu wa Mexico ambao wameonesha wasiwasi wao juu ya matumizi ya vinywaji vyenye sukari ambavyo vinapatika kwa urahisi sana hapa nchini kuwa ni jambo la hatari,

Pia tumezungumzi umuhimu wa taasisi hizi baada mwaka 2015 ziangalie namna kujipanga mambo kwa mapana zaidi katika kutokomeza magonjwa yaliyoanishwa,"amesema Dk Mwele.

Katika hatua nyingine Dk Mwele amechaguliwa kuwa Rais wa muda wa Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa cha afya za Jamii(IANPHI) Chapter ya Afrika ili kuwa na sauti moja katika mikutano ya kimataifa.
Mkutano wa taasisi hizo wa mwaka 2014 utafanyika katika nchi ya Morocco
Posted by MROKI On Wednesday, October 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo