NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI wa Afya na Ustawi
wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amewataka waganga
wa tiba asili washirikiane na wataalamu
wa utafiti ili kuwezesha upatikanaji wa dawa bora na salama.
Kauli hiyo ilitolewa
leo na Waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya tiba ya
asili ya mwafrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 31, lakini mwaka huu
hayakufanyika kutokana na uhaba wa fedha. Maadhimisho hayo yanatarajiwa
kufanyika mwakani kipindi katika hicho.
“ Tanzania tunayo mitidawa mingi na mingi haijafanyiwa kazi
katika utafit na kuweza kubaini uwezo wa kutibu magonjwa mbailmbali tatizo
lililopo ni jinsi gani mitidawa hiyo inweza kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora
na salama kwa watumiaji kwa kuziwekea mifumo ya huduma za afya ili kila mwenye
kuhitaji aweze kuzipata,” alisema Dk. Mwinyi .
Dk. Mwinyi aliwataka
waganga hao kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi
ya Utafiti wa Dawa za Asili
iliyokpo katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shiriki- (MUHAS).
Aliongeza kuwa
waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa wanatakiwa kufanya kazi kwa
kuelewana ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya utafiti kamili
kufanyika.
Aliitaja kauli mbiu
ya maadhimisho hayo kuwa ni ‘ Tiba Asili : Utafiti na Maendeleo’ kuwa inalenga
kutoa majukumu kwa waganaga wa tiba
asili na tiba mbadala katika sula zima la utafiti. Pili inatoa changamoto juu
ya uendelezaji wa taarifa za utafiti wa mitidawa katika kutafuta dawa ya kutibu
magonjwa mbalimbali.
Aidha aliwahimiza
waganga wa tiba asili kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na
huduma za afya.
0 comments:
Post a Comment