Watoto wa Mkulima wakipeana ushauri...!!! Muasisi na Mwendeshaji wa Mtandao huu wa Father Kidevu Blog, Mroki Mroki 'Father Kidevu' akimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (kulia) juu ya kilimo bora cha umwagiliaji. Father Kidevu alitembelea Shambani kwa Waziri Mkuukatika kijiji cha Zuzu kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma kujionea shughuli mbalimbali za kilimo ikiwepo ufugaji nyuki.
Waziri Mkuu Pinda, alimwambia Father Kidevu kuwa kilimo chenye tija hakihitaji eneo kubwa sana na pia Maji ni muhimu si kutegemea mvua ambazo hivi sasa si za uhakika. "Ukiwa na Kisima cha maji katika shamba lako hapo ni kila kitu, ardhi yeyote inaweza kubadilika"
Eneo la shamba la Migomba iliyostawi vizuri la Waziri Mkuu. Pinda amewaasa vijana kujiunga na kujikita katika kilimo kwani fursa hiyo ikitumiwa vyema inaweza kumpa kipato mtu kuliko hata ajira ya maofisini.
Zabibu zilizovunwa katika shamba la Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Zabibu hizi zipo za aina mbili za kutengenezea Mvinyo (Wine) na zile za Mezani (Zabibu za kula kawaida). Father Kidevu Blog imebaini kuwa Asilimia kubwa ya Zazibu zinazouzwa mitaani ni zabibu za kuzalishia Mvinyo kutokana na naldha iliyopo katika Zabibu za kula.
0 comments:
Post a Comment