Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali pamoja na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa tanki la maji katika kata ya Kagongwa Wilayani Kahama wakati alipoanza rasmi ziara yake ya siku nne katika mkoa wa shinyanga leo na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na za kukiimarisha chama katika mkoa huo, Katika picha wanaoshuhudia kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa tanki hilo la maji katika kata ya Kagongwa Hili niyo tanki linalojengwa katika kata ya Kagogwa wilayani Kahama Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akisoma ujumbe katika mabango yaliyoandikwa na wana CCM kuelezea kero zao Nape amepokea kero ya wanaCCM hao na kuahidi kulishughulikia mara moja. Umati uliojitokeza katika mkutano wa hadhara mjini Kahama. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kahama. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kahama leo. Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikbidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM Ndeke Mdaki katika kata ya Isaka Wilayani Kahama. Ndugu Ezekiel Maige mbunge wa Msalala akiwahutubia wananchi katika Kata ya Isaka Wilayani Kahama. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Kituo cha afya katika kata ya Mwendakulima kijiji cha Mwendakulima iliyojengwa na kampuni ya Kuchimba madini ya mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama , kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa mgodi wa Buzwagi Bw. Richard Otendo wa pili kutoka kulia. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mwakilishi wa mkuu wa mgodi wa Buzwagi Richard Otendo wakati alipotembelea jengo la kituo cha afya cha Mwendakulima lililojengwa na mgodi huo.
Hili ndilo jengo lenyewe. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananc hi katika kata ya Mwendakulima mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha kata hiyo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Diwani wa Kata hiyo kutoka TLP Bw. Ntabi Majabi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima.
Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kupanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima. Wana CCM wakiwa katika mkutano wa Ndani mjini Kahama.
Kikundi cha Sarakasi kikionyesha uwezo wao katika sarakasi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sinjita mjini Kahama.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAHAMA
0 comments:
Post a Comment