Meneja wa mauzo na usambazaji wa kampuni ya Samsung ,
Silvester Manyara, Bakari Maggid toka
bodi ya michezo ya kubahatisha na meneja mwakilishi wa Samsung nchini Kishor
Kumar wakiwa wameshika baaadhi ya bidhaa za kampuni hiyo zinazotolewa kwa
washindi wa droo inayofanyika kila mwezi.
Mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bakari Maggid (kushoto) akifurahia jambo na Meneja
wa mauzo na usambazaji wa kampuni ya Samsung , Silvester Manyara na meneja
mwakilishi wa Samsung nchini, Kishor Kumar wakati wa droo ya mshindi bidhaa za
Samsung iliyochezeshwa jana katika duka la kampuni hiyo lililopo Uchumi Plaza,
barabara ya Nyerere.
*************
Kwa mara nyingine tena Kampuni
ya Samsung Tanzania imechezesha droo ya mfumo wake wa “E-Warranty”, washindi
walitangazwa katika hafla iliyoandaliwa katika Ofisi zao katika Barabara ya
Pugu. Mfumo huu wa “E-Warranty ni mbinu inayotumiwa na Kampuni ya Samsung kama
jinsi ya kukumbana na bidhaa feki zinazopatikana kwenye soko la Tanzania.
Mfumo huo wa e-warranty unawasaidia wateja kujua
kama simu ya Samsung ni halali au ni feki. Wateja wanapaswa kusajali simu zao
pale wanapozinunua na hivyo kupata dhamana ya miezi 24.
Meneja
Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema “Mfumo wa E-Warranty
imeonyesha kwamba ni mbinu bora zaidi dhidi ya kukumbana na bidhaa feki kwani
wateja wengi wanasajili simu zao. Tunawahimiza wateja wetu waendele kutuunga mkono kwa kununu bidhaa
bora na kuzisajili na hivyo kupata nafasi ya kujishindia bidhaa kabambe za
Samsung katika droo zetu”.
Washindi wanaweza kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10:
Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32, laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na
simu 2 aina ya Galaxy Grand.
Bwana Kumar aliendelea
kusema “ Licha na kujua kama simu mteja anayotaka kununua ni bora au feki,
mfumo wa e-warranty unawasiadia wateja kujua kama simu hiyo inadhama ya miezi
24, kama simu hiyo inatafutwa au imeibiwa na kama simu hiyo ni mpya au
imeshatumika”.
Kujua kama simu ni halali, mteja anatakiwa kufuta
maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’ ikifuatiwa na alama ya nyota
(*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa na alama ya reli (#) na
kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa moja kwa moja kuelezea hadhi
ya simu hiyo ya Samsung.
“Mfumo huu wa e-warranty ulianzishwa haswa
kukabiliana na changamoto moto inayoikumba soko la simu za mkononi huku
Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu nyingi ni za bandia, za
wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana”, alisema Bwana, Kumar.
Bwana Kumar alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha
huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4
(iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa
ADH. ADH (Accidental Damage from Handling), ni huduma inayoilinda simu
hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na matumizi ya kawaida’.
Ilikujiunga na huduma ya ADH, wateja wanatakiwa
kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili untakiwa kufanywa ndani ya siku 30
tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa
muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure
pale ambapo itaharibika.
0 comments:
Post a Comment