Mratibu
wa maadhimisho ya unywaji wa maziwa mashuleni Iringa kutoka
kampuni ya Asas Bw Tony Adam katikati akizungumza na wanahabari
Iringa katika ofisi za IPC juu ya maadhimisho hayo ,kulia ni katibu
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bw Francis Godwin na
kushoto ni afisa habari wa kampuni ya maziwa ya Asas
Wanahabari wa vyombo mbali mbali wakimsikiliza kwa makini mratibu huyo
Na Francis Godwin, Iringa
WAKATI kesho ni maadhimisho ya siku ya unywaji maziwa duniani ,kampuni ya
maziwa ya Asas Dairies Limited Iringa inakusudia kuwanywesha maziwa
wanafunzi 30,000 wa shule za msingi katika Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa kama sehemu ya kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa
kunywa maziwa kwa afya .
Akizungumza
na wanahabari leo katika ofisi za IPC ,mratibu wa uhamasishaji unywaji maziwa mashuleni
kutoka kampuni ya ya maziwa ya Asas Bw Tony Adam alisema kuwa kuwa
wakati madhimisho ya unywaji maziwa kitaifa yanafanyika katika mkoa
wa Tanga ,Kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd yenye makao yake makuu
mkoani Iringa imelazimika kufanya maadhimisho hayo mjini Iringa kwa
kushirikiana na uongozi wa Manispaa ya Iringa.
Mratibu
huyo alisema kuwa shule zote za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
zitapata kupewa maziwa katika uwanja wa Samora mbele ya mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma .
PIa
alisema kuwa wanafunzi wote wa shule za msingi wenye miaka chini
ya 10 watashiriki katika mashindano ya uchoraji wa picha za rangi
zitakazobeba
ujumbe wa maziwa kwa mfano ng'ombe akila majani ama mtoto
akinywa maziwa .
Mbali
ya watoto kushindana kuchora pia watu wazima watapata kushiriki
semina itakayoelezea umuhimu wa unywaji wa maziwa na madhara ya
kutotumia maziwa katika mwili wa binadamu na kuwa semina hiyo
itahusisha pia wadau wa maziwa na viongozi wa mkoa na Manispaa ya
Iringa pamoja na wawakilishi wa taasisi zinazohusika na sekta ya maziwa
za zile bodi ya maziwa , lishe na
chakula nchini (TFNC).
Alisema
madhumuni makubwa ya madhimisho hayo ni kuamsha hisia za wakazi wa
Manispaa ya Iringa kuhusu umuhimu wa unywaji maziwa katika kujenga
afya ya mwili na kiakili zaidi.
Kwani
alisema kuwa kiwango cha unywaji wa
maziwa nchini bado ni wa kiwango cha chini sana cha wastani wa
lita 40 za maziwa kwa mtu kwa mwaka ambazo zimepanda lita 60 za
maziwa kwa mtu kwa mwaka ikilinganishwa na kiwango cha kimataifa
(WHO) cha lita 200 za maziwa kwa mtu kwa mwaka au kiwango cha
majirani zetu Kenya cha lita 120 za maziwa kwa mtu mmoja kwa mwaka .
Alisema
kuwa kiwango chetu hapa nchini ni sawa na na unywaji wa maziwa
cha pipa moja la maziwa kwa
mtu mmoja kwa mwaka huku dhamira ya kiwanda cha Asas Iringa ni
kuona kiwango hicho kinaongezeka kufikia lita 80 hadi 100 za
maziwa kwa mtu mmoja kwa mwaka ndani ya kipindi cha miaka 5 ijayo.
Mratibu
huyo alisema kuwa kiwanda hicho cha Asas Dairies Ltd
kimeendelea kufikisha bidhaa zake kwa wananchi wengi zaidi nchini
kwa kuhakikisha wanafikiwa na huduma zao na kutaja bidhaa
zinazozalishwa kuwa ni maziwa fresh,maziwa mgando ,Yogurts zenye
ladha mbali
mbali .
Aidha
ametaja kaulu mbio ya maadhimisho ya unywaji wa maziwa mashuleni
katika Manispaa ya Iringa kwa mwaka huu kuwa ni UNYWAJI WA MAZIWA
KILA SIKU SHULENI NI HAKI YA KILA MWANAFUNZI.
0 comments:
Post a Comment