Nafasi Ya Matangazo

August 27, 2013

 WAREMBO 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013, leo wanatarajiwa kukutana rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo wake shughuli itakayofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni waandaaji wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013, Hashim Lundenga alisema, mkutano kati ya waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini.
“Washiriki  wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali analotaka,” alisema.
 Leo washiriki hao walikuwa na semina maalumu kati ya washiriki hao na waandaaji wa mashindano haya ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Limited.
Baada ya kukutana na waandishi wa habari kesho, warembo hao wanatarajiwa kuanza ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.
Warembo hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo  mbalimbali yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.
Brigitte Alfred ndiye anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Meneja wa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi chote kile.
Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

 Warembo wakitoka katika ukumbi wa JETI 1 Hoteli ya Giraffe ambako leo walikuwa na semina.
 Warembo wakiwa katika pozi la picha
Mwalimu wa warembo hao Magdalena Roy ambaye ndiye anashikilia taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2012, akizungumza jambo na washiriki wa Redd's Miss Tanzania 2013.
Posted by MROKI On Tuesday, August 27, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo