Nafasi Ya Matangazo

August 27, 2013


MDHAMINI Mkuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ leo wanatarajia kukabidhi vifaa kwa timu shiriki za ligi hiyo katika hafla itakayofanyika hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
 
Katika hafla hiyo maalumu inayotarajiwa kuanza saa 4 asubuhi, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
 
Akithibitisha hilo, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema, hiyo ni kuashiria kukaribia kuanza rasmi kwa msimu wa Ligi Kuu ya Zanzibar wa 2013/3014.
 
“Kama tulivyoahidi kipindi tunaingia mkataba wa kudhamini ligi hii, kesho (leo) tutakabidhi zawadi kwa timu zote zishiriki za ligi hiyo, ambavyo vitakuwa ni vifaa bora kabisa.
 
“Pia tutatoa mipira itakayotumika katika ligi hiyo pamoja na jezi maalumu kwa waamuzi, kwani tunachotaka ni kuwa na ligi bora na iliyo na ushindani,” alisema.
 
Naye Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, watahakikisha wanaendelea kutoa udhamini uliotukuka kwa ajili ya kukuza michezo ndani ya Zanzibar.
 
“Ligi Kuu ya Grand Malt ndio inatarajiwa kuanza wiki ijayo na sisi tuko kwa ajili ya kuhakikisha inaafanikiwa zaidi,” alisema.
 
KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza kabisa toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
Kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini ligi hiyo hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.
Posted by MROKI On Tuesday, August 27, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo