Wakulima wa shayiri katika kata ya Ngare Nairobi mkoani Kilimanjaro, wakikagua shayiri ya mkulima mwenzao ambaye alipata mbegu kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kampuni
hiyo iliwatembelea wakulima hao wa kanda ya kaskazini na kujadili jinsi
ya kukuza kilimo cha zao hilo huku kampuni hiyo ikitatua matatizoyanayowakabili wakulima hao kwa kuwapatia pembejeo na kuwaahidi
kuwaletea mtaalam wa kupima udongo ili kujua ni mbolea gani dhabiti
itumike ili kupata mavuno yanayoridhisha..
Diwani wa kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha, mkoa wa Kilimanjaro akitoa maelekezo kwa wawakilishi wa Kampuni
ya Bia ya Serengeti ambao ni Menaja mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti, Imani Lwinga(wa pili kushoto) pamoja na Meneja kilimo
wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(wapili kulia) wakati walipotembelea
mashamba ya shayiri katika kata hiyo kwa lengo la kuwainua wakulima.
Menaja mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Imani Lwinga(kushoto) pamoja na Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(kulia) wakikagua shayiri katika shamba la Bora Msaki mmoja ya wakulima wanaonufaika na mradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoani Kilimanjaro katika kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha. Kampuni hiyo inaunga mkono kampeni ya Kilimo Kwanza kwa kuwapa mbegu na kuwahakikishia soko la kuridhisha wakulima wa shayiri kanda ya kaskazini.
0 comments:
Post a Comment