Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad.
|
****************
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la
makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa
kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na
chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka Januari hadi Machi mwaka huu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu
Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda
inayongoza kwa uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na
uanzishajiwa mpango wa damu salama wa kampeni ya
kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari katika jamii na kushirikisha wadau.
Aliwaomba
wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia
damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.
“Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi
kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC) na wadau wengine wa
Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)”
alisema Bw. Mwenda.
Bw.
Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani ambapo lengo la
kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa wa
damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683
Alisema
Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za
kiraia nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia
damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma kutoka chupa za
damu 2,560 mpaka chupa 3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.
Bw.
Mwenda alisema ushirikiano ni mdogo kati ya wahamasishaji wa
Mpango wa damu salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya
ya damu kidogo inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu
hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji na usambazaji wa damu.
Alisema
changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa za damu
kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu hivyo
kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.
Bw. Mwenda alisema Serikali kupitia Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005
ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote wanaohitaji.
Alisema shughuli za mpango ni pamoja na
uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na
usambazaji wa damu salama mahospitalini.
Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka
lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu
iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia
1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la
uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la
wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu
na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.
0 comments:
Post a Comment