NYOTA ya
mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada
ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu
wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa)
lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha
hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera
ya Tanzania kimataifa.
Katika
orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa
ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya
Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice
Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace
Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.
Flaviana
Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka
2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake
aliendelea na fani ya uanamitindo Afrika
kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika
makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko
Wilhelmina Models.
0 comments:
Post a Comment