Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na
Viongozi wa Steps (hawako pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa
mazungumzo juu ya maendeleo ya kazi za sanaa jijini Dar es Salaam.
Mtaalum Mshauri Bw.
Sanctus Mtsimbe akiomuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Mhe. Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) moja ya kazi yake iliyopitia taratibu zote na ambayo hakimiliki
ni yake mwenyewe.
Moja ya viongozi wa
Steps Entertainment Bw. Jairaj Damodaran akifafanua jambo wakati wa kikao na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
Kushoto ni Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamun Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni Prof. Hermas
Mwansoko wakisikiliza majadiliano wakati wa mazungumzo kati ya Steps na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara jijini Dar
es Salaam.
*********
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
WAZIRI wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amekutana na wadau wa Kampuni
ya Steps Entertainment na kuzungumza nao
juu ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini. Ujumbe huo wa Steps ulioongozwa na
Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki .
Katika mazungumzo hayo Dkt.
Fenella amegusia masuala ya uharamia katika kazi za filamu nchini na kutia mkazo katika
suala zima la maadili. Aidha Waziri ameeleza kuwa kuanza kwa urasimishwaji wa
tasnia ya filamu na muziki unaoendelea kutekelezwa nchini kutasaidia sana
kuondosha kazi zisizohalali.
Aidha, Dkt. Fenella
amewashauri wadau wa tasnia ya filamu
nchini washirikiane kikamilifu na Serikali katika kuendeleza na kukuza tasnia
ya filamu na pia kuhakikisha wasanii wananufaika na jasho lao. Aidha ameeleza
umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau na umma
kwa ujumla juu ya fursa nyingi zilizopo katika tasnia.
Kwa upande mwingine Waziri
Dkt. Fenella ameshauri pia kuwe na majumba maalum kwa ajili ya kuonyeshea
sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania pia amehamasisha wadau wa filamu kuanzisha majumba
hayo na ambao tayari wameanzisha kutoa fursa hiyo ili kuziendeleza kazi za
filamu za kitanzania.
“Kuwe na majumba ya kuonyeshea
sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania”. Alisema Dkt.
Fenella.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alibainisha kuwa kumekuwa na
ongezeko kubwa la filamu zinazowasilishwa kwa ukaguzi na pia wadau wameanza
kutumia stempu za TRA katika kazi za filamu na muziki ili kuzilinda kazi hizo.
Stampu zilianza kutolewa tangu mwezi Januari mwaka huu .
Kwa upande mwingine Mkurugenzi
Mkuu Bw. Dileshi Solanki wa Kampuni ya Steps Entertainment ameiahidi Serikali
kupitia Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Mukangara, kuendelea
kuendeleza tasnia ya filamu kwa kushirikiana kikamilifu na serikali na kupiga
vita uharamia dhidi ya filamu za kitanzania . Aidha wameiomba serikali
kuendelea kuwajengea mazingira mazuri.
0 comments:
Post a Comment